Home Blog

Vichekesho Mkutano wa Mandela na Nyerere Kule Ng’ambo ya Pili

1
Vichekesho vya Nyerere na Mandela

Nyerere:  Kama vile nakufananisha?
Mandela: Hata mimi naona sio sura ngeni?
Nyerere: We ndie Mandela eee?!
Mandela: Ndiyo mimi haswa miaka 14 ni mingi.
Nyerere: Sana!!.
Mandela: Sasa nitakaa wapi mbona hakueleweki huku?
Nyerere: We ngoja utapaelewa tu.
Nyerere: Eeh!! vipi huko Tanzania? ulitembelea hata hivi karibuni?

Mandela:

Eeeh! we acha tu, huko mara Zitto msaliti, mara Umeme mgawo miezi sita, mara mgomo wa Gesi haitoki Mtwara, mara kifo cha Mwangosi, mara Dawa za Kulevya,  mara Meno ya Tembo, mara kuchoma Makanisa, mara mabomu kwenye mikutano ya hadhara na makanisani, mara  Ufisadi, mara Dr. Ulimboka na Kibanda kung’olewa kucha na meno kwa plauzi, mara Division 5, mara Udini, mara ngumi Bungeni, mara kifo cha Dr Mvungi, mara tindikali kwa mapadri, mashehe na wageni, mara Kagame kuishambulia Tanznia, Petroli kuchakachuliwa, mara wengine wanasema eti Muungano ulioasisi unatokana na Visiwa vya Zimbabwe na Zanzibar na sio Tanganyika tena, mara muungano wa serikali tatu ndio unaotakiwa, mara Kigamboni kapewa Obama, mara Bushi na mke wake kaja Tanzania, Clinton na mke wake kaja Tanzania, Kamerun na mke wake kaja Tanzania, Xiing wa uchina kaja Tanzania, mara puttin wa Urusi kaja Tanzania. Yaani hekaya ni ndefu bora urudi ukayashuhudie mwenyewe.

Mara Mandela alipomrushia macho swahiba wake kumbe kashazimia saa nyingi

You can be charged for virtually everything. Kansiime Anne. African Comedy.

0

What!!? U have not Subscribed yet??? Eh nga you are a RISK -TAKER!!
NOW NEW CLIPS EVERY WEEK!!!
pls also

What a taxi ride! by Kansiime Anne – African Comed

0

What!!? U have not Subscribed yet??? Eh nga you are a RISK -TAKER!!
NOW NEW CLIPS EVERY WEEK!!!
pls also

Vichekesho vya Mchaga Kwenye Kisima

0
Mchaga Katika Kisima Kilichoachwa

Hebu fuatilia kichekesho hiki na angalia usivunjike mbavu

Kuna Mchaga mmoja kanasa kwenye kisima asubuhi na mapema akiwahi kibaruani. Kisima hicho kilitelekezwa na jirani yake

Baada ya maangaiko makubwa ya kumtoa, mmojawapo wa watoto wake alikuja na kamba na kumtupia ili waweze kumnasua kisimani.

Mahojiano yalikuwa hivi

Mtoto: Baba ebu daka hiyo kamba uing’ang’anie ili tukuvute mpaka utoke uko

Baba wa kichaga: Kwani hiyo kamba umenunua shilingi ngapi na kwa nani?

Mtoto: Nimenunua Shilingi elfu moja kwenye lile duka la mpare

Baba wa Kichaga: Alipatwa na mshangao haraka akajibu, Eyowii!! Amekuuzia ghali sana kijana, ebu rudisha na ukanunue kamba kwa Mosha anauza mia tano.

Wote: Wakashangaa, wakacheka na kuvunjika mbavu!

Kansiime Anne demands condolenses – African comedy

0

What!!? U have not Subscribed yet??? Eh nga you are a RISK -TAKER!!
NOW NEW CLIPS EVERY WEEK
pls also

Vichekesho vya Mume na Mke – Penzi la Pesa

2

MUME: Hallo my queen…

MKE: Nambiee..my darling

MUME: Nimekumiss honey.

MKE: Hata mie nimekumiss ile mbaya..

MUME: Samahani mke wangu leo sitaweza kurudi nyumbani.. nitakuja kesho asubuhi

MKE: Unasemaje?? na uishie hukohuko.. kalale kwa hao mahawara zako.. mwanaume mbaya wewe, kama sokwe.. sijui hata ni shetani gani alienishawishi hadi nikaolewa na sokwe kama wewe..

yaani najuta.. najuta.. sikupendi toka ndani ya moyo wangu..

sikupendi hata kidogo..naogopa hata watu kujua kuwa umenioa ..

naona aibu.

MUME: Punguza jazba mke wangu niko bank.. kuna foleni ndefu sana..

MKE: Ahh pole sana darling.. nakuonea huruma handsome wangu wa kipekee.. but baby usisahau kuniletea pesa kidogo.. ninashida na laki 2, alafu kuna ile elfu 70 anayonidai
mama amina leo alikuja kunikumbushia. nimekuandalia maji ya moto sweetie ukija uoge mume wangu kipenzi.. then ukumbuke kuniletea chips na kuku wa kuchoma gengeni.. nimeimiss sana.. nakupenda sana mfalme wangu..

MUME: Ni bank ya kuchangia damu.

MKE: Na wakutoe hiyo damu yote, bora ufe tu.. huna faida na si lolote.. nyooo… potelea mbali..mijitu mingine bhana..!!