Dk. Willibrod Slaa ashangaa kuteuliwa kwake kuwa balozi, akubali

0
1
Rais John Magufuli amemteua Katibu Mkuu wa zamani, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – , Dk. Willibrod Slaa kuwa balozi. za iliyotolewa jana na Ikulu ilisema Dk. Slaa ataapishwa baada ya taratibu zote kukamilika. Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa na Mwandishi wa Mwananchi maoni yake kuhusu uteuzi wa Rais, alijibu kwa ujumbe mfupi kupitia mtandao wa WhatsApp kuwa, "Mungu wangu, no comment". Baada ya hapo hakupatikana tena. Hata hivyo, baadaye akiongea na kituo cha televisheni cha Azam Tv, Dk. Slaa alisema amepata ya kuteuliwa kwake na kwamba amekubali kwa kuwa umefanywa na mkuu wa nchi. Dk Slaa aliiambia Azam Tv kuwa anamshukuru Rais Magufuli kwa kumteua ili aungane naye kujenga nchi na hivyo atafanya kazi kwa uwezo wake wote.
Chanzo. JamiiForums

Toa maoni yako juu ya Dk. Willibrod Slaa ashangaa kuteuliwa kwake kuwa balozi, akubali kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply