Kagame Akubaliwa Kutawala Tena Kwa Miaka 17 Hadi 2034

0
102
Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame 2015
Rwanda's President Paul Kagame speaks during the Emerging Markets Summit 2009 in London September 18, 2009. REUTERS/Luke MacGregor (BRITAIN POLITICS BUSINESS)

Wananchi wa Rwanda wamepiga kura ya kubadilisha katiba ili kumruhusu Rais wa sasa, Paul Kagame kugombea tena mpaka mwaka 2034. Kagame amekubaliwa na Wanyarwanda kwa asilimia 98 hii ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi nchi za nje. Hii ina maana Kagame atatawala tena Rwanda kwa miaka mingine 17. Tume ya uchaguzi ya Rwanda imesema kuwa hayo ni matokeo ya awali na matokeo kamili yatatangazwa yakishakamilika.

Kagame ambaye kwa sasa ana miaka 58 atastaafu urais wa Rwanda akiwa na miaka 75 kama kwa chaguzi zote atashinda.

Kura hii imesukumwa na ukweli kwamba Kagame amefanya vizuri sio tu ndani ya Rwanda bali pia hata nje ya Rwanda ukilinganisha na nchi nyingi kusini mwa jangwa la sahara.

Nchi ya Rwanda ni miongoni mwa nchi yenye serikali yenye nidhamu na uwajibikaji wa hali ya juu na ambayo inaendeshwa kwa uwazi na bila matukio ya rushwa na ufisadi.

Ripoti ya Transparency International ya mwaka 2014 imeipa Rwanda nafasi ya kwanza kati ya nchi za maziwa makuu na ya pili katika Afrika. Rwanda imekuwa ya 55 kati ya nchi 175 zilizofanyiwa utafiti kwa mwaka huo kwa kupata alama 49 wakati nchi ya Kenya ikishika nafasi ya 145/175 kwa kupata alama 25, Uganda ya 142/175 kwa kupata alama 26, Tanzania ya 119/175 kwa kupata alama 31, Burundi ya 159/175 kwa kupata alama 20, Zaire ya 154/175 kwa kupata alama 22.

Aidha nchi ya Botswana imekuwa nchi ya 31/175 na kuwa nchi ya kwanza Afrika kwa kupata alama 63

Kwa upande wa Dunia Denmark imetangazwa kuwa nchi safi ya kwanza kwa rushwa duniani ikipata alama 92.

Toa maoni yako juu ya Kagame Akubaliwa Kutawala Tena Kwa Miaka 17 Hadi 2034 kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply