Meseji za Vichekesho

15
74220
meseji ya vichekesho

Jamaa mmoja alimuaga mke wake wa ndoa kuwa anakwenda safari kumbe huku nyuma kapanga kusafiri na kujirusha na bi mdogo. Baada ya kujirusha kwa usiku mmmoja kesho yake akiwa ofisini aliamu kumtumia meseji ya shukrani bi mdogo na meseji ilikuwa hivi:

“Asante mpenzi kwa staili uliyonifanyia jana usiku, umekosha moyo wangu sitasahau mpenzi. Na mimi nitakutunza leo, miss you”

Kwa bahati mabaya bila kukusudia aliweka namba ya mke wake wa ndoa badala ya bi mdogo na alibofya kidude cha send. Meseji ilienda moja kwa moja kwa mke wake yaani waifu.
Jamaa kuona hivyo haraka akawahi ofisi za fokodam (kampuni ya simu) na kumuuliza karani kama anaweza kuzuia meseji isimfikie waifu wake.

Karani naye katoa mpya kwa kamuambia awahi kwenye mnara ili aweze kuzuia. Hata hivyo meseji hiyo ilimfikia waifu….

 

 

Toa maoni yako juu ya Meseji za Vichekesho kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

15 COMMENTS

Leave a Reply