Je wajua kuwa…


Vichekesho vya je wajuaJe wajua kuwa unaweza kutuma taarifa zako kwenye tovuti ya jewajua.com kwa kutumia dirisha la tuwasiliane?.  Tumia fursa hii kutangaza biashara yako kwa kuwahabarisha uma.

Kumb. Vigezo na masharti kuzingatiwa

Search the FAQ:

Je wajua| Askofu anamiliki hammer?
Jan. 18, 2010 by Sam Severua, Tanzania
Awali Risasi Jumamosi lilipenyezewa ‘tipu’ juu ya kuwepo kwa Askofu mmoja (jina tunalo), anayemiliki gari aina ya ‘Hammer’ inayokadiriwa kuwa na thamani ya ‘ngawira’ za kitanzania Milioni 250 na ‘ushee’ ambapo uchunguzi ulianza mara moja na kutengeneza kichwa cha habari hii. Katika ishu hiyo, baadhi ya waumini walilieleza gazeti hili kuwa, gari hilo analotumia Mtumishi huyo huku akivalia ‘krauni’ ya uaskofu, likitiwa mafuta ya shilingi elfu thelathini (30,000) haliwaki hivyo humlazimu kuweka ‘wese’ la shilingi laki tatu (300,000) ili kukamilisha mizunguko yake ya siku moja. Katika nusanusa ya makachero wetu ilibainika kwamba, mbali na baadhi ya watumishi hao kumiliki magari, majumba na vitu vya kifahari, lakini pia mavazi na mfumo wao wa maisha unawashangaza baadhi ya ‘kondoo’ wanaowaongoza. Ilisemekana pia kuwa, mmoja wa viongozi hao (naye jina tunalo), amekuwa akitinga madhabahuni na ‘pamba’ za mtoko mmoja zikiwa na thamani ya shilingi laki tano na nusu (550,000) huku akitoa ushuhuda kwa waumini wake kuwa, hayo ni matunda ya kumtumikia Mungu. Katika chimbua chimbua ya hapa na pale, mapaparazi wetu walitonywa pia kuwa, mmoja wa viongozi hao ambaye yeye hujitambulisha kuwa ni Nabii, akiwa katika harakati zozote barabarani hupewa ‘eskoti’ ya msururu wa magari na ving’ora kama ule wa rais wa nchi. Ernest Madewe, ambaye ni muumini wa moja ya makanisa ambayo kiongozi wake yuko kwenye listi hiyo, aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, kondoo wa Mungu wamekuwa ‘wakikamuliwa’ fedha bila kujali umasikini unaowakabili. Alisema: “Kuna wakati tunajaza fomu maalum za kueleza mali tulizonazo ili kuhakikisha tunatoa fungu la kumi linaloendana na kile tulichonacho bila kujali kuwa kuna baadhi yetu tuko hoi na hatuna kitu. “Suala la sadaka linapaswa kuwa siri ya mtu na Mungu wake, lakini kinachoshangaza, jamaa wanakaba kupita kiasi.” Baadhi ya maaskofu, wachungaji, walimu na manabii wanaosifika kwa kutoa huduma ya kiroho vizuri ni pamoja na Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water ‘kanisa la makuti’ lililopo Kawe na Mch. Getrude Lwakatare ‘Mama Lwakatare’ wa Kanisa la Assemblies of God la Mikocheni B, yote ya jijini Dar. Wengine ni Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel lenye makao yake makuu pembeni mwa Barabara ya Sam Nujoma, Josephat Mwingira wa Kanisa la Ephata Ministry na Askofu Silvester Gamanywa wa Huduma ya Hakuna Lisilowezekana, nayo ya jijini Dar. Listi hiyo ndefu inaungwa na Mch. Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufalme na Ufufuo lililopo Ubungo, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ wa Ubungo Kibangu na Nabii GeorDavie wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lenye makao yake makuu mkoani Arusha.

VN:R_N [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/5 (0 votes cast)

Je umependa huu ukurasa? Kama ni vipi, mtumie rafiki Au hifadhi sasa,
tell a friend
Kuhusu huu ukurasa na kujiandikisha ili utumiwe taarifa za blogu hili RSS feed.

2 Responses to Je Unapenda Kucheka?

  • Baraka Daniel Kubuka says:

    Hakuna mwalimu mkali kama ulimwengu usiombe kufunzwa naye kwani hana msamaha wala maswali wala majibu juta kukutana naye!!

  • Msafiri says:

    Hao ni viongozi wa dini au ni wauzaji wa madawa kulevya,kwasababu dini yoyote inawausia watu kuwa na imani na wanyonge na wasiojiweza kiuchumi ili kuwasaidia na sio kuwalazimisha watoe michango wakati wenyewe wanahitaji kuchangiwa na kusaidiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

Jiunge Kupokea Taarifa

Weka barua pepe yako hapa kupokea taarifa mpya zinapotokea


 

RSS News

Waliotutembelea

Waliotutembelea Leo: 30
Jana: 113
Mwezi huu: 1567
Jumla: 21734
Walioko hewani Sasa: 1
Waliosoma leo: 457
Waliosoma jana: 1732
Mwezi huu: 27714
Jumla: 277095

Picha Maalum