Vituko vya Konda wa Daladala na Abiria

5
8373
Vituko vya Konda wa Daladala na Abiria

Kwa wale mnaotumia sana usafiri wa umma au daladala utakuwa umekumbana na mojawapo ya ya vituko vya makonda na abiria wa daladala kama ifuatavyo

 1. Mlokole; konda weka nyimbo za Yesu
 2. Konda; Yesu bado hajatoa albam.
 3. Matozi; humu ndani joto
 4. Konda; kapande friji
 5. Abiria; kuna siti?
 6. Konda; Kwani hawa walioko wamekalia madumu?
 7. Sistaduu: Konda unanibana
 8. Konda; hiyo suruali inakubana mbona husemi!
 9. Mama: sikai siti za mwisho
 10. Konda; Kwani hizo siti za mwisho ziko nje ya gari?
 11. Abiria : we konda  vipi kuwa  kama umeenda  shule
 12. Konda: Mimi ndiyo kwanza nimetoka shule

Kama una mengine tafadhali ututumie na tutakuwekea kiunganishi cha blogu au web yako hapa bure.

 

 

Toa maoni yako juu ya Vituko vya Konda wa Daladala na Abiria kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

5 COMMENTS

Leave a Reply