Askari Kanzu Mmoja Akumbana Na Kipigo Kikali Muhimbili

0
178

Wakati hayo yakitokea inadaiwa kuwa Askari Kanzu mmoja alikumbana na kipigo kikali kutoka kwa madaktari hapo Muhimbili kwa kile kilochodaiwa kutambuliwa na Dkt Ulimboka kuwa mmoja wa watu walio mjeruhi.

Pia inadaiwa kuwa Askari huyo aliingia chooni na kufanya mawasiliano na wenzake huku Madaktari hao wakimsikiliza na kutokana na alichokua akiongea chooni humo ndipo alipotoka aliambulia kichapo kikali.

Pia baadhi ya madkatari na wauguzi walikuwa wakisukuma gari alilokuwa amepanda Dkt Ulimboka huku wakiimba nyimbo za Umoja na Mshikamano Daima miongoni mwao.

Hali ya ulinzi ilikuwa kali Hospitalini hapo kwani Picha zilikuwa haziruhusiwi kupigwa.

Toa maoni yako juu ya Askari Kanzu Mmoja Akumbana Na Kipigo Kikali Muhimbili kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

ACHA MAONI

Please enter your comment!
Please enter your name here