AZAM FC Yaiadhibu Bidvest Wits ya Afrika ya Kusini kwa 3-0 Nyumbani Kwao

0
144
CAF Confederation 13 Machi 2016 Bidvest Wits VS AZAM FC

Bidvest Wits imeangukia pua kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kupatiwa kichapo cha mabao 3-0 na AZAM FC ya Tanzania. Huo ulikuwa ni mchuano wa mzunguko wa kwanza wa kuwania kombe la washindi lijulikanalo kama CAF Confederation Cup.

AZAMA walipata mabao yote matatu ndani ya dakika 10. Mabao hayo yalifungwa na Salum Abubakar katika dakika ya 51 kwa mkwaju wa mbali baada ya kukutana na mpira wa kona uliokolewa na mchezaji wa WIts.

Dakika sita baadaye Shomari Kapombe aliongeza bao la pili kwa AZAM baada ya kutumia vyema mpira alioupata kutokana na pasi mbovu ya nyuma ailiyokuwa akirudishiwa Jethren Barr kutoka kwa Tebogo Moerane.

Baadaye tena Kapteni wa AZAM, John Boko alifunga goli la tatu baada ya safu wa walinzi wa Wits kufanya marking mbovu.

Wachezaji:

Bidvest Wits: Barr, Nhlapo, Khumalo, Lecki, Sheppard, Bhasera, Motshwari, Mosiatlhaga, Moerane, Pule, Lupeta.

Benchi la akiba: Mbanjwa, Hlatshwayo, Klate, Mkatshana, Pelembe, Jordan and Sekese.

Azam FC: Manula, Bocco, Wawa, Nyoni, Kapombe, Singano, Mkami, Kipre, Kavumbagu, Salum and Moris.

Toa maoni yako juu ya AZAM FC Yaiadhibu Bidvest Wits ya Afrika ya Kusini kwa 3-0 Nyumbani Kwao kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply