Daraja la Dumila, Morogoro Laharibiwa na Mafuriko

0
1412
Daraja la Moro - Dodoma2

Wasafiri wengi wemekwama Dumila Morogoro wakitokea Mwanza Shinyanga, Kahama, Dodoma nk na kwa upande wa pili wakitokea Dar, Morogoro, nk kwa sababu ya daraja linalounganisha Morogoro na Dodoma la Dumila kuharibiwa vibaya na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea. Malori mengi pia yamekwama na kusababisha adha kubwa kwa wasafiri, wafanyabiashara na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuingia hasara kwani imewabidi kuwaamuru madereva kuchukua njia ya mzunguko kupitia Kilosa.Wee fikiria kama ungekuwa ndio wewe unabeba sangara zaoko kuwa biashara Dar au ndio unawahi mkutano au deal la biashara dar, au Mwanza. We fikiria ndio mwenye basi unaingia gharama ya kulizungusha basi au lori kupitia njia ndefu na hivyo kuingiza hasara kubwa namna hiyo kwa tatizo ambalo linajulikana miaka nenda rudi.

Matatizo ya araja hili ni la muda mrefu. Karibu kila mwaka kuna tatizo pale.

Toa maoni yako juu ya Daraja la Dumila, Morogoro Laharibiwa na Mafuriko kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

ACHA MAONI

Please enter your comment!
Please enter your name here