Dk. Ulimboka Asimulia Tukio la Kutekwa na Kupigwa

0
44

Akisumulia tukio hilo Dkt Ulimboka alisema kuwa  jana usiku alipigiwa simu na mtu aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea naye, na ndipo walipopanga kuonana katika eneo la Leaders Kinondoni.

Dk Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa tabu, aliendelea kusimulia kuwa wakati akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa akifahamiana naye kabla, alikuwa na wasiwasi kwani kila mara alikuwa akipokea simu na kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.

Alisema baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha Polisi na kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.

Dk. Ulimboka alisema kuwa wakiwa njiani walimpiga, na kumfikisha katika msitu huo wa pande na kuendelea kumpiga paka alipoteza fahamu.

Toa maoni yako juu ya Dk. Ulimboka Asimulia Tukio la Kutekwa na Kupigwa kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

ACHA MAONI

Please enter your comment!
Please enter your name here