FAO Kujitoa Sheria Za Mifuko Ya Hifadhi Ya Jamii

1
603
sheria mpya ya mafao ya wafanyakazi Tanzania

sheria mpya ya mafao ya wafanyakazi TanzaniaKumb. Na. AE/164/334/Vol.II/2 20 JULAI, 2012

Makamu wa Rais, Corporate Affairs

Barrick Gold

S.L.P 1081

Dar-es-Salaam

UFAFANUZI KUHUS FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

 1. Kama mtakumbuka za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na tarehe 13 Aprili, 2012. hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.
 2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.
 3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.
 4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.
 5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia
 6. Wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika
 7. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.
 8. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu
 9. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.
 10. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii

Irene Isaka

MKURUGENZI MKUU

Toa maoni yako juu ya FAO Kujitoa Sheria Za Mifuko Ya Hifadhi Ya Jamii kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Oni moja

 1. Jamani serikali itufikirie wanachi, kwa sasa maisha yamekuwa magumu sana , kuzuia fao la kujitoa ni kuendelza umaskini kwa mwanachi. Kwa kweli Raisi wetu apitie upya sheria hii aliyo pitishea

Leave a Reply