Hadithi ya Mkware na Mtoto wa Tajiri

Hapo zamani za kale walitoke vijana wawili waliokua marafiki sana. Mmoja akiitwa “mtoto wa tajiri” na mwingine “ndugu mkware”.. Waliitwa “Boys 2 Men” kwa jinsi walivyoshibana. Mtoto wa Tajiri baba yake alikuwa na mali nyingi lakini “ndugu mkware” alikuwa mtoto wa Fukara baba yake akiwa Area Commisioner.

Mtoto wa tajiri akawa anatumia fedha zake kumsaidia “ndugu mkware”. Walisoma pamoja, wakaenda jeshini pamoja hata kwenye siasa waliingia pamoja. Mwaka 1995 wakakubaliana wakachukue fomu ya Ufalme, mmoja akipata mwenzie anakuwa “Waziri mkubwa” afu “anamsapoti” mwenzie baadae akigombea Ufalme.

Wakakubaliana lakini “ndugu mkware” alikua hana hela. Yule mtoto wa tajiri akamwambia mkware usijali tutatumia hela zangu maana lengo letu ni moja. Akakodi ndege (Private Jet) wakapanda wawili hadi Idodomya. Wakapokelewa kwa shangwe kubwa.

Wajumbe wa “mkutano mkubwa” wakawa wanamtaka zaidi yule mtoto wa Tajiri. Yalipochujwa majina matano na “Kamati Kubwa: bahati nzuri wote wawili wakapenya. Yalipochujwa kubaki matatu, Mtu mmoja aitwae “Mwalimu mkuu” akaagiza yule mtoto wa tajiri akatwe. Akakatwa.

Wakabaki watatu wakapelekwa Kwenye “mkutano mkubwa”. Mmoja kati ya hao watatu ni “ndugu mkware”. Yule mtoto wa tajiri akahamishia wafuasi wake wote kwa rafiki yake ili ashinde. Ndugu Mkware akashinda lakini “Mwalimu mkuu” alikuwa hamkubali kabisa ndugu mkware. Akasema “KATA HUYU BADO HAJAKUA.”. Akakatwa akapewa ushindi ndugu mmoja aitwae “mtu mfupi”

Basi “mtu mfupi” akawa Mfalme na akawateua wale marafiki wawili wawe maawaziri. Wale marafiki wakakubaliana mwaka 2005 wagombee tena Ufalme na mmoja akipata ampe support mwenzie kipindi kijacho.

Mwaka 2005 wakachukua fomu ya Ufalme wote wawili lakini “ndugu mkware” akamwambia yule mtoto wa tajiri, niunge mkono mimi halafu nitakussuport mimi nikitoka.

Yule mtoto wa tajiri akamuuliza “mkware” una gari ngapi za kampeni, akasema sina. Akamwuliza tena umeshatengeneza network na watu wangapi wa kukusupport? akasema bado sijafikiria. Akamuuliza tena una pesa kiasi gani za kufanya kampeni, ndugu “mkware” akasema sipo vizuri.

Yule mtoto wa tajiri akamwambia mbona huna kitu halafu unataka kugombea “Ufalme?” utawezaje? Mkware akamwambia mwenzie “naomba nisaidie tafadhali”. Basi yule mtoto wa tajiri alikua amejaliwa hekima na utu akakubali kumsaidia ndugu mkware. akampa fedha, akamtengenezea timu ya mikakati ya ushindi, akamfanyia fund rising, akamfanyia kampeni nzuri hadi mkware akashinda.

Baada ya kushinda ndugu mkware akapiga “dili la pesa nyingi” akamuomba mtoto wa tajiri amsaidie kuficha siri. Wakati huo mtoto wa tajiri alikua “waziri mkubwa”.. Lakini lile dili likaharibika.. Kivumbi kikatokea “bondeni”.. Mkware akamuita yule mtoto wa tajiri na kumuomba ajiuzulu nafasi yake ya “uwaziri mkubwa” ili kuokoa jahazi. Jamaa kwa sababu ya urafiki wao akakubali kubeba mzigo usio wake akajiuzulu.

Baada ya hapo mkware akaanza kumpakazia mwenzie vitu vya uongo ili kumchafua. Akawa anamsema vibaya akiwa kando lakini akiwa karibu anamsifia. Mkware akaanza tabia za kinafiki kwa “mtoto wa tajiri”.

Mkware alipokaribia kustaafu yule mtoto wa tajiri akaenda kumwambia unakumbuka ahadi yetu? Nilikuunga mkono kwa hali na mali. Kwa nguvu na pesa, sasa ni zamu yako kuniunga mkono.

Ndugu Mkware akakataa akamwambia wewe ni mchafu. Mtoto wa tajiri akamwambia Mkware mimi si mchafu. Unajua wazi mimi nilikubali kuchafuka ili wewe upone. Niligeuka mbuzi wa kafara kwa ajili yako, kwanini unataka kunisaliti?

Kumbe “mkware” alishaandaa mdogo wake ili amwachie kiti cha Ufalme. Huyo mdogo wake alikua mkulima “MTAMA”. Na aliaga kule “bondeni” akasema “sitaki tena kuwakilisha wakulima wa Mtama, nataka ufalme”. Wananchi wa ile nchi wakapaza sauti wakasema “hii nchi sio ya familia, ukimpa mdogo wako nafasi hatumchagui kuwa mfalme wetu”.. Basi ndugu mkware akaogopa akacha mpango wa kumpa ndugu yake Ufalme.

Mtoto wa tajiri akachukua fomu ya Ufalme, mara ndugu mkware akiwa amejaa roho ya ukatili na bila kukumbuka fadhila akawaambia wale wenzie mkateni huyu. Mtoto wa Tajiri akakatwa. Basi akahuzunika sana kuwa rafiki yzke amemsaliti. Rafiki aliyemsaidia tangu ujana wake, rafiki aliyemjali kuliko ndugu yake, rafiki yske aliyempenda na kumthamini lakini leo amemsaliti.

Akasikitika sana. akamwambia “mkware” ASANTE KWA KUNISALITI, mimi nahama nyumba. Ndugu mkware akadhani mtoto wa tajiri anatania akamjibu kwa kejeli “hama tu”.

Basi mtoto wa tajiri akahama nyumba akaenda nyumba ya jirani. Alipofika akapokelewa kwa Shangwe na vigelegele. Akapewa nafasi nyingine ya kuutafuta Ufalme. Na muda si mrefu atashinda na atakuwa mfalme kisha ataweka wazi usaliti wa ndugu “mkware”

Na watu waliposikia hadithi hii wakasikitika na kusema “Hakika Wakware si watu”

Toa maoni yako juu ya Hadithi ya Mkware na Mtoto wa Tajiri kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply