ICC Yaitahadharisha Tanzania

0
1175
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC-Bibi Fatou Bensouda

Mwendesha Mashtaka Mkuu(ICC) Bibi Fatou Bensouda aitahadharisha Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015.

Juzi alipokuwa Arusha Mh. Edward Lowassa mgombea wa urais kupitia UKAWA lizungumzia swala la watawala na dola kugoma kuachia mamlaka na kusisitiza kuwa atawashitaki katika mahakama ya kimataifa, ICC. The Hague….

Haikupita hata masaa 72 mwendesha mashitaka mkuu Bibi Fatou Bensouda amesikika akiongea na kituo cha televisheni cha Aljazeera maneno yafuatayo (Aljazeera, kwenye segment ya Africa Today)…..

Nanunukuu

“The ICC is keenly watching and following closely what is transpiring in Tanzania’s forthcoming General elections and as we did in countries like Kenya, Ivory Coast and Congo we shall expeditiously act with immediate effect on any cases of human rights violations”.

– Fatou Bensouda, The Hague.

Akiiimaanisha kuwa

“ICC inaangalia na kufuatilia kwa karibu yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu ujao nchini Tanzania na kama tulivyofanya katika nchi kama Kenya, Ivory Coast na Kongo, tutashughulikia  kwa ufanisi na kwa uharaka tukio lolote la ukiukwaji wa haki za binadamu”

– Fatou Bensouda, The Hague.

Hayo yamejiri leo ambapo Mwendesha mashitaka huyo alipokuwa anaongelea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini Uganda mapema mwakani na Tanzania mwisho wa mwaka huu.

ICC wanastahili kupewa pongezi kwa tahadhari hii ambayo imekuja kwa wakati wake huku wanasiasa nchini Tanzania wakiwa wameshaanza kutoa kauli zinazoashiria ukiukwaji wa haki za binadamu na hatimaye umwagaji wa damu.

Kauli hizo ni pamoja na

Tutashinda ikibidi kwa goli la mkono

– Nape Nnauye – CCM

Tutashinda kwa vyovyote vile

– Jakay Kikwete – CCM

Tutashinda Asubuhi

– Edward Lowassa – CHADEMA

Aidha matukio kama ya kuwapiga mabomu wafuasi wa wagombea Arusha na Mwanza ni dalili mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

ACHA MAONI

Please enter your comment!
Please enter your name here