Jakaya Mrisho Kikwete Azindua Vitambulisho Vya Taifa

0
1424
Jakaya Mrisho Kikwete Azindua Vitambulisho vya Taifa

Jakaya Mrisho Kikwete Azindua Vitambulisho vya TaifaLeo mkuu wa kaya Dr Jakaya Mrisho Kikwete amezindua vitambulisho vya Taifa ambazo vimetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa kabisa ya digitali inayoitwa “SmartCard”

Kwanza kabisa sipingi vitambulisho hivi kabisa ila nina hoja;

Tanzania ina zaidi ya watu 44 milioni na katika idadi hiyo zaidi ya 80% wanaishi vijijini

Pia zaidi ya 95% wanaishi chini ya dola moja kwa siku au kwa maneno mengine chini ya Shs 1600/siku. Sijui ni kwa asilimia ngapi lakini leo hii watanzania wengi wanaganga njaa, yaani hawajui mlo utakaofuata wataupata au la. Kwa maneno mengine wanapigania maisha ya mlo mmoja kwa siku tu. Pia wanapigania maisha kwa huduma mbovu na zilizokufa za afya.

Mfano nasikia huko Shinyanga baadhi ya sehemu ukienda na debe la matobolwa unapatiwa hekari nzima bure. Hii inaonyesha jinsi issue ya njaa Tanzania ilivyo kubwa.

Sasa hiki kitambulisho cha mahela mengi sana ambayo kwa kweli ni ya kisasa kuliko hata ukisasa wa Watanzania wenyewe japo ina faida nyingi kwa sababu itakuwa ikidhibitiwa kielectroniki, lakini kwa mlalahoi itamsaidia nini?

Faida

Itakuwa na ujumla wa tawkimu binafsi za Mtanzania na hivyo kuifanya serikali kuwa rahisi kufuatilia tabia, kazi, makazi na mienendo yote ya mtu. Itaisadia Serikali kuwa na takwimu halisi zaidi za watu na pia kuthibiti uhalifu kwani kitambulisho hizi huwezi kufoji kama hivi vya manual ambazo ziko kwenye majadala yaliyojaa vumbi.

Pia itawasaidia TRA kujua wewe na mimi tunafanya kazi gani na hivyo kuweza kufuatilia kama unalipa kodi au la

Kwa ufupi zaidi ya faida lukuki ya hivi vitambulisho ila hii ya kuthibiti uhalifu na walipa kodi ndio kubwa kuliko zingine

Sasa hoja yangu iko hapa

Mtanzania wa kawaida anayepigania uhai wake kwani hata mlo unaofuata hajui ataupataje, akiwa na hii kitambulisho itamsaidia au hii kitambulisho ni kwa jili ya kuisadia serikali kukusanya kodi tu?

Ukisema Serikali ikikusanya kodi kubwa itaweza kumshibisha huyu mtanzania anayepigania maisha yake kwa mlo mmoja tu je, hii kidogo ambayo serikali imekuwa ikikusanya na kuruhusu ufisadi na pesa nyingi kuhamishiwa kwenye mabenki ya Uswisi na chache kutumika kuporomosha magorofa ya kifisadi nchini si watafanyiza zaidi wakipata fursa ya kukusanya kodi kubwa zaidi?

 

Najua wakazi wenye upeo wa Dar tu, au katikati ya JIJI la Arusha, Mwanza, Zanzibar nk wataona hii hoja haina mashiko. Lakini hebu rudi kule kijijini kabisa halafu wewe na familia yako ni ile inayoishi chini ya 1600 kwa siku, matumaini gani utaweka katika hiki kitambulisho.

Pia kama hutaki kwenda kijijini, basi hebu jifanye wewe ni huyo mlalahoi wa mwisho hapo mjini ulipo ambapo hujui hata kama leo utakula nini na hii ndio staili ya kawaida ya maisha yako? Je utakuwa na matumaini gani kwa hiki kitambulisho ambayo unakwenda kupewa muda mfupi ujao iliyotengenezwa kwa mapesa mengi kibao?

Kwa wale wanaopaa na FASJET, EMIRATE na KLM na kwa wale wanatembea huku na kule nchini Uganda, Kenya, Rwanda, DRC nk najua inafaida kubwa kwenu. Ila kwa hao zaidi ya 80% wasiotembea kwa sababu ya ufukara wa kutupwa itawasaidia kupata mlo ambao ndio hitaji lao kubwa?

Sijui kama hoja yangu imepotoka au la

Natoa hoja

Maelezo zaidi:-

NIDA kuongeza mda wa zoezi la vitambulisho vya taifaNIDA kuongeza mda wa zoezi la vitambulisho vya taifa
Mamlaka ya vitambulisho vya taifa imetoa taarifa za kuongezwa muda wa wiki moja wa zoezi hilo jijini dar es salaam na sasa litamalizika Agosti 6 mwaka huu.

 

Tanzania: Usajili wa watu kwa ajili ya vitambulisho vya taifaTanzania: Usajili wa watu kwa ajili ya vitambulisho vya taifa
Mamlaka ya vitambulisho Tanzania (NIDA) imeanza rasmi zoezi la utambuzi na usajili wa watu kwa ajili kupatiwa vitambulisho vya taifa. Zoezi hili litaendeshwa kwa awamu nane ambapo awamu ya kwanza ni kwa watumishi wa umma. Kwa maelezo zaidi tembelea: www.nida.go.tz

 

Zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya taifa leo.Zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya taifa leo.
Muda uliongezwa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA umekamilika huku katika baadhi ya vituo kukiwa bado kuna idadi kubwa ya watu ambao hawajajiandikisha.

 

voa mitaani-vitambulisho vya taifa.voa mitaani-vitambulisho vya taifa.

 

Hotuba ya Dr. Slaa ya Kwanza katika Mikutano ya Operesheni Sangara IfakaraHotuba ya Dr. Slaa ya Kwanza katika Mikutano ya Operesheni Sangara Ifakara
Katika Hotuba hii Dr. Slaa amezungumzia swala la Polisi kunyanyasa raia, kutekwa kwa Dr. Steven Ulimboka, na Umuhimu wa Wananchi kujiandikisha na Kupata Vitambulisho vya Uraia

 

CUF YAZINDUWA OPERESHENI YA MCHAKAMCHAKA HADI 2015CUF YAZINDUWA OPERESHENI YA MCHAKAMCHAKA HADI 2015
Chama cha wananchi CUF kimeitaka serikali kutumia mradi wa vitambulisho vya taifa kuangalia namna ya kuwawezesha wananchi wake Kunufaika na mapato yanayotokana na rasilimali za taifa ikiwemo gesi.

 

NIDA
http://www.nida.go.tz/
Karibu na asante kwa kutumia muda wako kutembelea tovuti yetu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Nimefarijika kufahamu kwamba watu wengi

Faida na Umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa
http://www.nida.go.tz/swahili/index.php%3Foption%3Dcom_content%26view%3Darticle%26id%3D80%26Itemid%3D113
Faida na Umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa. Vitambulisho vya Taifa ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Vitasaidia kuongeza wigo wa

Raia Mwema – Fomu za Vitambulisho vya Taifa zaanza kutolewa Dar
http://www.raiamwema.co.tz/fomu-za-vitambulisho-vya-taifa-zaanza-kutolewa-dar
18 Jul 2012 MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema imeanza kutoa fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa kwa wakazi wa Dar es

ZOEZI LA KUANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA LINA …
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/zoezi-la-kuandikisha-vitambulisho-vya-taifa-lina-kasoro-lukuki
31 Jul 2012 Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Mwaimu. KWANZA tumshukuru Mungu kwa kutuweka hai leo na kubwa zaidi kwa kutuwezesha kukutana katika

News Alert: JK:vitambulisho vya taifa kutumika kupigia kura
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/397158-jk-vitambulisho-vya-taifa-kutumika-kupigia-kura.html
SOURCE:TBC HIYO KAULI NINA MASHAKA NAYO MAANA TUMESHAZOEA KUDANGANYWA.SIJASEMA RAIS MUONGO ila sijui sijui.

Vitambulisho vipya vya uraia vya Tanzania kuimarisha usalama …
http://sabahionline.com/sw/articles/hoa/articles/features/2012/07/12/feature-02
12 Jul 2012 Mpango wa kadi za vitambulisho vipya vya taifa nchini Tanzania umeanza mwezi uliopita jijini Dar es Salaam katika jitihada za kuimarisha

ASILIMIA 80 WAJIANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA KUSINI …
http://www.fullshangweblog.com/2012/10/25/asilimia-80-wajiandikisha-vitambulisho-vya-taifa-kusini-unguja/
25 Okt 2012 Zaiidi ya aslimia 80 ya wakazi wa wilaya ya Kusini Unguja Zanzibar wamejitokeza kujiandikisha kupata vitambulisho vya Taifa wengi wao

 

Toa maoni yako juu ya Jakaya Mrisho Kikwete Azindua Vitambulisho Vya Taifa kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply