Mbunge wa Kahama James Lembeli CCM Atangaza Rasmi Kuhamia CHADEMA

0
926
James Lembeli Mbunge wa Kahama Ahamia CHADEMAMbunge w Kahama kupitia CCM, Mh. James Lembeli ambaye alikuwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili ametangaza rasmi kukihama chama cha mapinduzi CCM na kuhamia Cham,a cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA .
“Nimetafakari, nimezungumza na mama yangu kwa zaidi ya saa kumi. mke wangu na watoto wangu, na kwa kusikia kilio cha wananchi wa Jimbo la zamani la Kahama nimeamua kutangaza kuanzia leo kwamba natangaza kujiondoa uanachama wangu ndani ya CCM” – James Lembeli.
“Nilikipenda lakini nimelazimika kuchukua uamuzi huu, najua nawakera wengi lakini nawaomba waangalie hali ambayo Viongozi wa CCM Wilaya ya Kahama wamesababisha niamue uamuzi huu mgumu.
“Kuanzia leo najiunga na CHADEMA. Namshukuru Rais Kikwete, nafikiri atakuwa mtu wa kwanza kuamini haya ninayosema, mwaka 2010 mizengwe iliyofanyika lengo lake ilikuwa kukata jina langu, kila mtu anafahamu Rais mwenyewe aliwahi kuniambia lakini Rais Kikwete ndiye aliyerudisha jina langu. Ninaahidi nitaendelea kufanya kazi nae mahali popote, na MUNGU naomba anisaidie niweze kuvuka salama katika haya”- James Lembeli.

Toa maoni yako juu ya Mbunge wa Kahama James Lembeli CCM Atangaza Rasmi Kuhamia CHADEMA kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply