Je wajua historia ya tajiri wa pili duniani Warren Buffet?

0
5331
Je wajua historia ya Tajiri wa pili Duniani Warren Buffet
Je wajua historia ya Tajiri wa pili Duniani Warren Buffet

Je wajua historia ya Tajiri wa pili Duniani Warren Buffet
Je wajua historia ya Tajiri wa pili Duniani Warren Buffet

Je wajua historia ya tajiri wa pili duniani Warren Buffet? Yeye anamiliki zaidi ya dola za kimarekani bilioni 50 na ameshachangia zaidi ya billion 30. Haya ndio baadhi ya mambo yake muhimu kuzingatia:

 1. Alinunua shea za kwanza akiwa na miaka 11 tu. Sasa anajuta kuwa alichelewa kununua shea
 2. Alinunua kashamba kadogo akiwa na miaka 14 tu kwa fedha alizodunduliza kwa kusambaza magazeti
 3. Bado anaishi katika kijumba chake kisicho na fensi cha vyumba vitatu mpaka sasa iliyopo katika mji mdogo wa Omaha. Nyumba hiyo aliinunua miaka 50 iliyopita wakati anaoa. Anadai nyumba hiyo ina kila kitu anachohitaji kwa hiyo haitaji nyumba zaidi
 4. Anaendesha gari lake mwenyewe na hana dereva wala mlinzi
 5. Hasafiri kamwe na ndege binafsi japo anamiliki kampuni ya ndege kubwa kuliko zote duniani
 6. Kampuni yake ya Berkshire inamiliki makampuni 63. Huandika barua moja kila mwaka kwa wakurugenzi wa hizo kampuni akiwapo mwelekeo tu. Hafanyi mikutano wala kuwaita wakurugenzi mara kwa mara.
 7. Amewapa wakurugenzi wake masharti mawili tu
  1. Usipoteze pesa za wenye hisa
  2. Usisahau sharti la kwanza
  3. Hajichanganyi sana na jamii ya matajiri, maisha yake baada ya kuoa ni pop corn na kuangalia TV tu
  4. Warren Buffet habebi simu wala hana kompyuta kwenye dawati lake
  5. Billgates (Tajiri wa pili dunuani baada ya …wa Mexico ) alikutana nae kwa mara ya kwanza miaka 5 iliyopita. Billgates alidhani hana mambo yanayolandana na Warren Buffet, kwa hiyo alipanga kuonana nae kwa nusu saa tu lakini walipokutana walilonga kwa masaa zaidi ya kumi (10) na tangu hapo Billgates akawa mfuasi wa karibu wa Waren Buffet

Ushauri wake kwa vijana ni huu

 1. Kaa mbali na kadi za kusugua au mtandaoni yaani credit cards (Yeye anaziita mikopo ya benki) na uwekeze kwa wewe mwenyewe
 2. Pesa hazikumuumba mtu, bali mtu ndie aliyeziumba pesa
 3. Ishi maisha yako rahisi na halisi kama ulivyo
 4. Usitende yale wengine wayasemayo, bali wasikilize na wewe fanya unayojisikia ni mazuri
 5. Usihatamie vitu vyenye majina, vaa vitu unavyoona vinakupa raha
 6. Usitumie vibaya pesa zako, tumia tu pale kuna uhitaji
 7. Baada ya yote, hayo ni maisha yako kwanini uwape wengine wayaongoze maisha yako?

Maisha mazuri sio lazima yawepo katika vitu vizuri. Maisha rahisi na halisi ndio masiha mazuri

Toa maoni yako juu ya Je wajua historia ya tajiri wa pili duniani Warren Buffet? kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply