Kagame Kumchukia Kikwette ni Kwa sababu ya M23

0
1987
Askari Jasusi wa m23 Akiminywa Ili Aseme
Askari Jasusi wa m23 Akiminywa Ili Aseme
Askari Jasusi wa m23 Akiminywa Ili Aseme
Askari Jasusi wa m23 Akiminywa Ili Aseme

Haina shaka, Rasi wa Rwanda Paul Kagame kumchukia Kikwette kwa sababu ya ushauri tu haingii akilini. Niliwaza nikawazuia kwanini Kagame kang’aka aliposhauriwa kukutana na waasi wa FDLR

Kitendo cha kupeleka wanajeshi Kongo kulinda amani kumemuudhi sana Paul Kagame
kupeleka wanajeshi Kongo kupambana na M23 ni sawa na kupeleka wanajeshi Rwanda kupambana na Kagame. Na hii ndio nyuma ya sababu ya Kagame kumshambulia Kikwete alipomshauri akae na waasi hao kukubaliana ili kuleta amani ya kudumu katika eneo la maziwa makuu.
Kagame kapata pa kulipukia na kutapikia, na ndio maana hakukataa tu ushauri bali alitusi na kutaja kupigana. Hata mdogo atajua kuwa hasira ya Kagame sio ule ushauri wa Kikwete, bali ni hasira ya kupeleka wanajeshi Kongo kuwapiga ndugu zake waliokuwa wanamsaidia kutanua mipaka ya Rwanda kwa kisingizio cha Wanyamulenge wa Goma ambao kwa miaka mingi wametengwa na serikali ya Kinshasa.
M23 wakishinda kuimiliki Goma na Kivu watadai aidha uhuru kamili au kuwa sehemu ya Rwanda na Au Uganda.
M23 wakishindwa ni pigo kwa Kagame na washirika wengine. Sasa majeshi ya Tanzania na yale ya Afrika ya Kusini pamoja na Kongo yameanza mashambulizi ya kuwondoa M23 huko Kivuu ya Kaskazini na baadaye kusini mpaka Goma yote imekombolewa.
Je Kagame ataamua kulipeleka Jeshi lake kupigana na majeshi ya Tanzania huko Goma. Hilo bado limejificha. Je Kagame alimaanisha kumpa kichapo Kikwette ni huko Goma au kuna sehemu nyingine? Bado nalo ni kitendawili.
Lakini ukweli ni huu, Tanzania kupeleka askari huko Goma kumemuudhi sana Kagame na kuamua kumtapikia Kikwette kwa kisingizio ya ushauri wa kukutana na FLDR

Toa maoni yako juu ya Kagame Kumchukia Kikwette ni Kwa sababu ya M23 kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply