Kagame na Kikwete Wakishiriki Mkutano wa ICGLR Kampala Uganda 5 Septemba 2013

Kagame na Kikwete Wakisalimiana Kwenye Mkutano wa ICGR Kampala Uganda 5 Septemba 2013 Kwa Nyuso Zenye Jumbe Tofauti

Kagame na Kikwete Wakisalimiana Kwenye Mkutano wa ICGR Kampala Uganda 5 Septemba 2013 Kwa Nyuso Zenye Jumbe Tofauti

Picha hizi zinawaonyesha Paul Kagame ambaye ni Rais wa Rwanda na Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Tanzania wakishiriki mkutano wa ICGLR ambao kwa kirefu ni International Conference on the Great Lakes Region uliofanyika huko Kampala Uganda mnamo tarehe 5 Septemba 2013 ambao uliandaliwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda (Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki) kuzungumzia amani katika Maziwa makuu na hasa amani katika Kongo.

Viongozi hao wawili walipata pia muda wa kujadili namna ya kuboresha mahusiano ya muda mrefu kati ya nchi hizo mbili ambao ulienda vizuri kabisa. Mkutano huo umeondoa hofu iliyotanda kwa kuwepo na uwezekano wa nchi hizo mbili kuingia kwenye vita.

Ikumbukwe kuwa kwa takriban miezi minne iliyopita Rais wa Rwanda na mwenzake wa Tanzania wamekuwa katika hali ya uhasama hasa pale Raia wa Tanzania Ndg Jakaya Mrisho Kikwete alipowashauri marais wa Kongo, Uganda na Rwanda kukaa meza moja na waasi wanaopigana na serikali zao kuzungumza kwa lengo la kupatana ili kuleta amani katika eneo la maziwa makuu kitu ambayo mwenzake aling’aka na kuanza kutoa matamshi makali, magumu, kashfa na hata matusi. Hali hiyo haikuishia kwa Kagame tu bali hata baadhi ya mawaziri na maofisa wa serikali yake walisikika nao kwa nyakati tofauti wakitoa maneno makali dhidi ya Kikwete.

Paul Kagame na Jakaya Mrisho Kikwete Wasalimiana Uso kwa Uso Uganda

Paul Kagame na Jakaya Mrisho Kikwete Wasalimiana Uso kwa Uso Uganda

Paul Kagame na Jakaya Mrisho Kikwete Wakishiriki Mkutano wa ICGR Kampala Uganda 5 Septemba 2013 Paul Kagame na Jakaya Mrisho Kikwete Wakishiriki Mkutano wa ICGLR1 Kampala Uganda 5 Septemba 2013

Toa maoni yako juu ya Kagame na Kikwete Wakishiriki Mkutano wa ICGLR Kampala Uganda 5 Septemba 2013 kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply