Kichekesho cha Jamaa Mmoja na Nyumba Ndogo

0
5569
meseji ya nyumba ndogo kwenda kwa waifu

Kuna jamaa mmoja kwa muda mrefu alikuwa na mke kwa siri katika jiji la Ar. Siku moja katika kutenga muda wa kutosha wa kujirusha na bi jamaa kapanga safari ya kikazi na kumuaga mke wake kuwa anakwenda Dar kikazi nzima. Kumbe huku nyuma alipanga kutanua na bi .

Baada ya starehe za usiku wa jana yake na bi huyo, jamaa akiwa ofisini aliamua kumtumia meseji ya kushukuru bi

Jamaa katuma meseji hii:

“Asante baby kwa staili ya jana, ilikuwa kali sana na nimeipenda. Ndio maana nakupenda wewe kuliko wanawake wote duniani” na kuituma.

Baada ya kutuma jamaa kagundua kakosea namba na ilienda kwa waifu, yaani kwa mke wa ndoa

Jamaa katika kuhaha kuzuia meseji isimfikie mke wake alikwenda kwa wahudumu wa VodaCom ili kuomba msaada wa kuzuia meseji na mazungumzo yakawa hivi:

Jamaa: Kuna meseji nilikuwa niitume kwa bi mdogo kwa bahati mbaya imekwenda kwa waifu wangu, je mnaweza kuizuia?

Mhudumu: Wahi kwenye mnara

Toa maoni yako juu ya Kichekesho cha Jamaa Mmoja na Nyumba Ndogo kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply