Kichekesho cha Mchungaji na Mhudumu wa Bar

1
14456
mchungaji na bia

Mchungaji mmoja wa kipentekoste aliingia bar moja hapo Dar ili ahudumiwe kinywaji.

Mhudumu alipofika kwenye meza yake Mchungaji alimuagiza kinywaji:

Mchungaji: nipe bia ya kilimanjaro ya baridi
Mhudumu kwa sababu ya mambo mengi alipofika kaunta akasahau kama aliagizwa bia ya kilimanjaro moto au baridi.

Alimrudia na kumuuliza

Mhudumu: Samahani Mchungaji, hivi uliniagiza bia ya kilimanjaro ya moto au baridi?

Mchungaji akafadhaika kwa vile mhudumu alimtambua kuwa ni mchungaji naye haraka akamjibu hivi:

Mchungaji: nimesema maji ya kilimanjaro baridi.

Toa maoni yako juu ya Kichekesho cha Mchungaji na Mhudumu wa Bar kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

1 COMMENT

Leave a Reply