Kichekesho cha Mwanasheria Kijana na Fundi wa Simu

0
1289
Kichekesho cha mwanasheria na mteja


Jamaa mmoja mwanasheria mchanga kutoka chuo kikuu aliamua kujiajiri kwa kufungua kiofisi kidogo. 


Siku moja alimuona kijana mtanashati akiiwa anakuja ofisini kwake. Alipokaribia jamaa kachukua simu ya mezani na kuanza kuongea. 


Jamaa: Ile deni langu la dola elfu 50 mtanilipa lini?.


Jamaa kwenye simu: Tutakulipa mwisho wa mwezi bosi.


Jamaa: Hapana, ninazihitaji haraka kwani wiki ijayo nitakuwa na safari ya kwenda Marekani na nitapitia Uholanzi kulipia lile gari langu la dola elfu 90.


Jamaa wa kwenye simu: Mbona akaunti yako hatuna!


Jamaa: Wewe ingiza tu kwenye akaunti ile ile mliyonitumia dola laki moja mwezi ulipita.


Alipomaliza kuongea kwenye simu jamaa akamgeukia mgeni wake


Jamaa: Samahani mteja kwa kukuchelewesha, unajua nina mambo mengi sana


Mgeni: Samahani usijali, mimi ni fundi wa TTCL, nimekuja kurekebisha laini kwa sababu haikuwa hewani tangu juzi

Toa maoni yako juu ya Kichekesho cha Mwanasheria Kijana na Fundi wa Simu kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply