Kichekesho cha Kimombo na Meseji za Kimapenzi

8
35626
Simu na Meseji za Mapenzi

Njemba moja wa mjini alitumiwa meseji na rafiki yake wa kiume ambaye kwa bahati mbaya hakuhifadhi namba yake ya simu yake kwenye simkadi yake. Kutokana na urefu wa meseji ikashindwa kuonekana yote mwishoni ikaandika

‘some text missing…’

kwa vile jamaa kimombo hakishuki hivyo maneno ya mwisho hakuelewa maana yake lakini akahisi litakuwa neno la kimapenzi miss you kutoka kwa mchumba wake

Ili naye aonekane mjanja na anakijua kimombo akajibu hivi,

“some text missing too dear”

 

Kumbe ile message ilitoka kwa rafiki yake wa kiume

 

Jamaa ilibidi acheke tuu kwa sababu ya majibu ya swahiba wake

 

Toa maoni yako juu ya Kichekesho cha Kimombo na Meseji za Kimapenzi kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

8 COMMENTS

Leave a Reply