Lady JayDee akerwa kuzushiwa kutundikwa mimba

0
93

Lady Jaydee
Lady JayDee ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Forever ameibuka na kuonyesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya mashabiki wake wa Instagram ambao alidai waliichukulia vibaya post ya picha yenye kusema kuwa tumbo lake limevimba baada ya kupata msosi wa maana na mzuri.

Imebidi nifute post Ili nielezee upya.Hivi watu hamuelewi kiswahili au ni nini ??? Nimesema tumbo limevimba sababu ya sahani,nikimaanisha mlo na nili post nakula hapo awali Sasa hayo maneno mengine yanatokea wapi? Au niwe naandika kichina? Kwani mliambiwa nitazaa Rais atakayewatoa katika shida zote mpaka mnishikilie mimba mimba..Hebu niacheni basi khaaa Nisiishi Kisa mimba? Aisee mnaboa sana. Basi niueni Kisa sijazaa Ili niwaondolee kero kabisa.

aliandika Jide

Toa maoni yako juu ya Lady JayDee akerwa kuzushiwa kutundikwa mimba kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply