Lowassa Kuhamia CHADEMA, Dr Slaa Akataa, Mbowe, Ndesamburo, Mtei Sawa

2
3410

BREAKING NEWS
——————————–
Edward Ngoyai yuko mbioni kukamilisha mazungumzo na viongozi wakuu wa ili kukihamia chama hicho baada ya jina lake kuenguliwa katika kinyang’anyiro cha kugombea urais wa kupitia

Hata hivyo ujio wake huo umekigawa chama baada ya Katibu mkuu wa ambaye ndiye mgombea mtarajiwa kukataa katu katu uamuzi wa mwenyekiti wa Chama Freeman Mbowe wa kumuomba kuhamia

hali ndani ya imezidi kuwa tmbaya baada ya Dr. SLAA kutishia kukihama chama  kama MBOWE ataendelea kumshawishi na Kumuomba ajiunge na Chama hicho ili awe Mgombea wao wa Urais.

Dr. SLAA ameonyesha msimamo huo Muda mfupi kabla ya LOWASSA hajazungumza na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Masaki kuhusiana na mpango wake huo wa kukihama na kuhamia CHADEMA .

Dr Slaa amedai kwamba yeye hakubaliani na MBOWE kwenye mpango wake huo wa kumleta LOWASSA CHADEMA.

Hata hivyo chanzo chetu cha karibu na MBOWE imethibitisha kwamba MWENYEKITI wao huyo yupo tayari hata kumfukuza Chamani SLAA ili LOWASSA awe Mgombea wao. anasema MBOWE anaamini kwamba LOWASSA ataiwezesha CHADEMA kukiangusha .

Timu ya maandalizi ya LOWASSA imeamua kuahirisha mkutano wao na Waandishi wa Habari uliokuwa ufanyike leo saa Tano asubuhi ili kumpa Mbowe nafasi kama alivyoomba ili kwanza wamalize tofauti zilizojitokeza Kati yake na Dr Slaa.

Sambamba na huu mvutano Ikumbukwe pia kwamba hivi Sasa Dr. Slaa ana mvutano mwingine na viongozi wenzake wa UKAWA ambapo analazimisha yeye ndio awe Mgombea kupitia UKAWA.

Tayari Mzee Edwin Mtei ametumiwa ndege Moshi ili aje Dar kumshawishi Dr Slaa akubali kumpisha LOWASA kugombea urais Kupitia CHADEMA.

Hadi tunakwenda mtamboni mazungumzo baina ya Lowassa, Mzee Mtei, Mbowe na Ndesamburo yalikuwa bado yakiendelea.

Toa maoni yako juu ya Lowassa Kuhamia CHADEMA, Dr Slaa Akataa, Mbowe, Ndesamburo, Mtei Sawa kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

2 MAONI

Leave a Reply