Vichekesho vya Mchaga Kwenye Kisima

0
8509
Mchaga Katika Kisima Kilichoachwa

Hebu fuatilia kichekesho hiki na angalia usivunjike mbavu

Kuna Mchaga mmoja kanasa kwenye kisima asubuhi na mapema akiwahi kibaruani. Kisima hicho kilitelekezwa na jirani yake

Baada ya maangaiko makubwa ya kumtoa, mmojawapo wa watoto wake alikuja na kamba na kumtupia ili waweze kumnasua kisimani.

Mahojiano yalikuwa hivi

Mtoto: Baba ebu daka hiyo kamba uing’ang’anie ili tukuvute mpaka utoke uko

Baba wa kichaga: Kwani hiyo kamba umenunua shilingi ngapi na kwa nani?

Mtoto: Nimenunua Shilingi elfu moja kwenye lile duka la mpare

Baba wa Kichaga: Alipatwa na mshangao haraka akajibu, Eyowii!! Amekuuzia ghali sana kijana, ebu rudisha na ukanunue kamba kwa Mosha anauza mia tano.

Wote: Wakashangaa, wakacheka na kuvunjika mbavu!

Toa maoni yako juu ya Vichekesho vya Mchaga Kwenye Kisima kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply