Mh Zitto Kabwe Kuwasilisha Muswada Binafsi wa Kufuta Sheria Kandamizi ya Magazeti 1976

1
196
Mh Zitto Zuberi Kabwe na Muswada Binafsi wa Sheria Kandamizi ya Magazeti 1976

Mh. Mbunge wa Kigoma kaskazini, waziri kivuli wa fedha na mwenyeketi wa kamati ya ya uwekezaji wa umma Zuberi Zitto Kabwe anakusudia kupeleka muswaada binafsi wa kufuta kandamizi ya magazeti ya 1976.

ya Magazeti (The Newspaper Act 1976) inampa mamlaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzuia chapisho lolote linalotengenezwa hapa nchini ama kuingizwa kutoka nje ya nchi ambalo linaweza kuhatarisha matakwa ya nchi.  hii vilevile inampa mamlaka Waziri anayeshughulikia mambo ya habari kuzuia kuchapishwa kwa toleo lolote la gazeti, na kwamba itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote atakayechapisha, kuuza ama kusambaza gazeti hilo baada ya amri ya Waziri kutolewa.

Akiongea kwenye blogu yake Zitto Kabwe anasema,

“Nimetoa taarifa rasmi kwa katibu wa kwa mujibu wa kanuni za kwamba katika mkutano ujao wa nitawasilisha muswada binafsi wa sheria kufanya marekebisho ya sheria ya magazeti kwa lengo la kuifuta kabisa sheria hiyo.”

Aliendelea kusema kuwa madhumuni ya muswada huo ni;   

“kufuta sheria ya magazeti ya mwaka 1976 kwa sababu inakinzana na Katiba ya Nchi kuhusu haki za Raia kupata habari na kwamba iliorodheshwa na tume ya Nyalali ni sheria kandamizi’

Muswada wenyewe nitauwalisilisha siku ya ijumaa ili uchapwe kwenye gazeti la Serikali uweze kuingia kwenye shughuli za zitakazoanza tarehe 15 Oktoba 2013 kwa ngazi ya kamati.

TAARIFA YA KUWASILISHA MUSWADA BINAFSI WA SHERIA BUNGENI

Sheria ya magazeti ya 1976 inaenda kinyume na Katiba ya nchi Ibara ya 18 ya  Haki ya Uhuru wa Mawazo inayosema

18.- (1)  Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru

kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,

kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo

chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa

mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2)  Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu

matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu

kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala

muhimu kwa jamii.

Toa maoni yako juu ya Mh Zitto Kabwe Kuwasilisha Muswada Binafsi wa Kufuta Sheria Kandamizi ya Magazeti 1976 kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Oni moja

 1. MUSWADA BINAFSI KUFUTA SHERIA YA MAGAZETI YA 1976

  Napenda kuujulisha umma kwamba leo Ijumaa tarehe 4 Oktoba, 2013 nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge muswada binafsi Bungeni kufuta Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.

  Changamoto iliyopo ni Sheria mbadala ya vyombo vya habari baada ya Sheria ya sasa kufutwa. Hata hivyo wadau wa habari kama Baraza la Habari Tanzania wameshafanyia kazi suala hili kwa muda mrefu sana na wana mawazo kuhusu sheria mbadala. Nimejulishwa kuwa muswada wa sheria mpya ya habari tayari upo. Kwa hiyo katika mchakato wa kujadili muswada binafsi wa kufuta sheria ya magazeti ya mwaka 1976 mabadiliko yanaweza kufanywa ili kutunga sheria mpya. Hatua ya kwanza ni kuifuta sheria hii kandamizi ambayo kiukweli tumechukua muda mrefu sana na baada ya madhara makubwa kufikia hatua ya muswada wa kuifuta.

  Nimeamua kutumia njia za kawaida za kuwasilisha muswada na kuepuka njia ya dharura ili kujenga mazingira ya wadau wa habari kushiriki vya kutosha katika mabadiliko yanayotakiwa. Njia ya dharura ni ya haraka lakini huziba fursa za kupata maoni ya wadau ambao kimsingi ndio wenye sheria yenyewe haswa. Hivyo nimepeleka muswada leo ili uchapwe kwenye gazeti la Serikali (GN) kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kisha usomwe kwa mara ya kwanza, uende kwa wadau kwa mjadala na marekebisho na kisha kusomwa kwa mara ya pili na kupitishwa na Bunge.

  Ikumbukwe kuwa juhudi za kufuta sheria hii ni juhudi za wadau wa tasnia ya habari na ni juhudi walizofanya kwa muda mrefu sana. Mimi kama Mbunge ninawasilisha tu kwa sababu taratibu zetu za kuandika sheria zinataka ama Serikali, Kamati ya Bunge au Mbunge kuwasilisha muswada. Kwa muda mrefu tumewaangusha wana habari kwa kutosukuma vya kutosha mabadiliko waliyokuwa wanayapigania. Hata hivyo, kuna msemo wa kihindi ‘asubuhi huanza pale unapoamka’. Sasa tuchukue hatua za kufuta sheria hii kandamizi.

  Zitto Kabwe,Mb

  Kigoma Kaskazini

Leave a Reply