Mkutano wa UKAWA Buguruni na Ukimya wa Dr Slaa

0
969
Kile kikao cha viongozi wa UKAWA ambacho nimeripoti kwenye moja ya mada zangu leo kuwa kinafanyika Buguruni, Makao Makuu ya Ofisi za CUF kimemalizika muda mfupi uliopita. Katika kikao hicho, Ajenda zilikuwa Mbili

  1. Maandalizi ya Uteuzi wa Mgombea Urais na Mgombea Mwenza
  2. Ukimya wa Dr Slaa na John Mnyika

1. AGENDA YA KWANZA: UTEUZI WA MGOMBEA URAIS NA MGOMBEA MWENZA
Kwa upande wa ajenda ya Kwanza, kikao kilipata taarifa ya mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya . Kwamba, kimemaliza mchakato wa kumpata mgombea wake ambapo Edward Lowasa amepita bila kupingwa. Kutokana na tukio hilo, walitoa rai ya kuendelea na mchakato wa kumpata mgombea wa UKAWA.

Mwenyekiti wa , Freeman Mbowe aliwaeleza wajumbe kuwa kutokana na mashauriano waliyofanya huko nyuma, hatarajii kuona mjadala wa kumpata mgombea Urais wa UKAWA unazuka tena hali itakayoleta mgawanyiko baina yao. Kutokana na hali hiyo, alimuomba Prof. Lipumba ambaye ni mgombea wa CUF kujiondoa kwenye uchaguzi huo na kumwachia Edward Lowasa wa . Pia aliwaomba NCCR Mageuzi kupitia Mwenyekiti wake, James Mbatia kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho ili hatimaye wabaki na mgombea mmoja tu ambaye ni Edward Lowasa.

Baada ya majadiliano, wajumbe wa UKAWA kutokana na ombi la Lowasa kama lilivyowasilishwa na Mbowe waliridhia Lowasa ndiye awe mgombea wa UKAWA. Kutokana na hali hiyo, taratibu zinaendelea za kumtangaza Lowasa kuwa mgombea wa UKAWA na huenda tukio hilo litafanyika tarehe 4 au 5 jijini Dar ws Salaam.

Kwa upande wa nafasi ya Mgombea Mwenza, Mwenyekiti wa , Freeman Mbowe aliomba kubatilisha maamuzi ya kumteua Juma Duni Haji kuwa Mgombea Mwenza. Wajumbe walipohoji kuhusu hilo, Mbowe alisema kuwa kwa vile wamekubaliana kuwa mgombea Urais atakuwa Lowasa, mgombea wao ametoa mapendekezo ya mtu ambaye atafanyanaye kazi. Kwamba, Lowasa anampendekeza Ismail Jusa na si Juma Duni Haji kama walivyopendekeza hapo awali.

Taarifa za chini ya kapeti zinasema kuwa Juma Duni Haji amekataliwa na Lowasa kwa vile ana misimamo mikali hivyo Lowasa anahisi kwamba huenda wakashindwa kuelewana kwenye baadhi ya mambo. Kutokana na hali hiyo, Lowasa amempendekeza Ismail Jussa ambaye anammudu na wanaongea lugha moja. Ijapokuwa hawajakubaliana juu ya nafasi hiyo, ila ni dhahiri kuwa ni Jusa ndiye atakuwa Mgombea Mwenza kwa vile hakuna hoja au ombi lililotolewa na Lowasa likakataliwa.

2. AGENDA YA PILI: UKIMYA WA DR SLAA NA JOHN MNYIKA
Imeelezwa ndani ya kikao hicho kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa kwa sasa hatekelezi majukumu yake na kwamba ni zaidi ya wiki sasa haonekani na hapatikani kwenye simu. Kwamba, hali hiyo imetokea baada ya CHADEMA kumpendekeza Lowasa kuwa mgombea Urais. Kikao kilijulishwa kuwa mengi yanasemwa kwenye mitandao ya kijamii na taarifa iliyowashtua zaidi ni ile iliyoandikwa na Dr Slaa mwenyewe akimshutumu mwana CHADEMA mwenzake, Yeriko . Kwamba, taarifa hiyo imewashtua sana viongozi wa UKAWA na kwamba ni vema jitihada zikafanyika zaidi za kumshawishi ili asihame chama kwani akifanya hivyo umoja huo utakuwa hatarini.

Freeman Mbowe alisema kuwa Edward Lowasa ameonesha nia ya kutaka kuzungumza na Dr Slaa. Hata hivyo, alisema kuwa kuna ugumu wa kumfikia kwa vile hana mawasiliano ya simu na kwamba kila kitu kinachoendelea juu ya Dr Slaa sharti kifahamike na Mke wake. Kutokana na ugumu huo, Maalim Seif Sharif Hamad aliombwa aende kwa Dr Slaa kesho ama Keshokutwa ili akafanye naye mazungumzo na kumsihi abaki ndani ya CHADEMA. Maalim Seif amekubali ombi hilo na atashirikiana na baadhi ya wazee wa CHADEMA akiwemo Mzee Edwin Mtei.

Wadau, ni mengi yamezungumzwa kwenye kikao hicho. Ila haya niliyowasilisha ndiyo yaliyotawala kwenye kikao hicho.

Chanzo: JamiiForums.com Jukwaa la Siasa

Toa maoni yako juu ya Mkutano wa UKAWA Buguruni na Ukimya wa Dr Slaa kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply