Mtekaji wa Dk Ulimboka Huyu Hapa

0
945
Mtekaji wa Dk Ulimboka Akamatwa

Mtekaji wa Dk Ulimboka AkamatwaGazeti la MwanaHalisi toleo la Jumatano, 25, Julai 2012 limeandika kwa kina maelezo ya waliohusika na utekaji, utesaji na kujeruhiwa sana kwa kiongozi wa jumuiya ya madaktari Tanzania, Dr Steven Ulimboka mnamo tarehe 26 Juni 2012. Katika taarifa hiyo, majina ya Ramadhani Ighondu (RAMA) ambaye ni afisa usalama wa Taifa limetajwa kuhusika na mawasiliano ya mara kwa mara na hatimaye kupanga mkutano pale Leaders Club ambako Dk Ulimboka alitekwa na kulazimishwa kuingia kwenye gari, kupelekwa kwenye pori la Mabwepande. Majina mengine yaliyotajwa ambayo RAMA alikuwa akiwasiliana nao punde alipompigia Dk Ulimboka ni Buruani Ntilongwa (0712359533), Moshi Marungu Shabani (0761132663 na 0655162663)

Nakwambia ndugu yangu, kila pale ambapo Rama alifanya mawasiliano na Dk Ulimboka utaona hapohapo alifanya mawasiliano na Abdallah Kunja na NtilongwaHawa ni watu muhimu sana kwenye sakata hili. Taarifa zimeeleza.

Taarifa zinazidi kueleza kuwa simu ya bwana Rama iliingizwa salio la Sh. 252849. hili ni salio kubwa kwa mwaka huu.

Majina mengine ambayo Rama alikuwa akiwasiliano nao kabla Dk Ulimboka hajatekwa ni:

Mohamed Hassan (0655524444)

Shomari Kondo (0714666304

Optat Jacob Marandu (0716611625

Mbega Hisbert (0715222778)

Baada ya tukio Rama aliacha kutumia hiyo namba ya 0713760473 na kuanza kutumia namba zifuatazo

0714293425

0717030405

0713510585

0715466995

Dk Ulimboka alitekwa na kuteswa sana kwenye mojawapo ya majumba ya kificho na kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande nje ya jiji la Dar es salaam.

Rama anafanya kazi idara ya usalama wa Taifa chini ya Naibu mkurugenzi wa usalama anayeshughulikia siasa Jack Zoka. Zoka anatajwa katika njama zilizozagaa hivi karibuni za kutaka kuangamiza maisha ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroad Slaa, Mbunge wa jimbo la Ubungo, Mh John Mnyika na wengine wanaodaiwa ni wakosoaji wakubwa wa serikali.

Taarifa hizi zinakuja wiki moja baada ya kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova kutangaza kumshikilia nna kumpeleka mahakamani anayedaiwa kuhusika na utekaji nyara na utesaji wa Dk Ulimboka.

Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa Joshua malundi, raia wa Kenya ndiye aliyehusika na utekaji huo ambaye alishikwa alipokwendas kutubu katika kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mch Josephat Gwajima. Mch Gwajima alikana hilo na kuidai serikali iseme ukweli.

Mchungaji Gwajima aliaambia waumini wake kuwa

“Kwanza huyo mtu hakuja kwetu kutubu.. kama kutubu kwani kule kwao Kenya hakuna Mungu?”

Maelezo zaidi gazeti la mwanaHalisi la Tarehe 25, Jumatano Julai 2012
Toa maoni yako juu ya Mtekaji wa Dk Ulimboka Huyu Hapa kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply