Namna ya Kutambua Utapeli wa MPESA

0
1493

UTAPELI VODACOM MPESA TANZANIA

Leo nimetumiwa ujumbe huu hapa chini kutoka kwenye namba ya 0756868160

BN84BG705 Imethibitishwa
Umepokea Tsh50,000 kutoka kwa AIZA  MOLEII
Tarehe 17/5/15 saa 12:23 PM
Salio lako la M-PESA ni Tsh50,0000

Mtumaji alidai amenitumia MPESA kwa bahati mbaya kwani alikuwa akimtumia rafiki yake halafu akakosea ikaja kwangu. Alinisihi nimrudishie

Mimi nilimjibu awasiliane na VoDacom halafu yeye akasisitiza ni mtumie tu. Hapo hapo nikapatwa na wasiwasi nikasema ngoja nikachunguze huo ujumbe wa MPESA.

Nilipofungua kwenye sehemu ya kusomea message kwanza nikakuta ujumbe wenyewe umetoka kwenye namba ya 0756868160 badala ya namba maalum ya MPESA ambayo huwa inaandika tu neno M-PESA.Nilipocheki salio nikakuta sio sawa na salio la kwenye akaunti yangu ya MPESA. Halafu nikachunguza saa ya kutuma ni tofauti na iliyoandikwa kwenye ujumbe.

Nikaona niwashirikishe huu ujanja wa mjini ili ndugu zangu msiingizwe mjini na wakora

Mambo muhimu ya kuangalia ili kujua kama MPESA ni ya kitapeli

  1. Lazima ije na kichwa cha ujumbe M-PESA na wala sio namba ya simu
  2. Lazima tarehe na saa ya MPESA ziendane na tarehe na saa ya ujumbe kutumwa
  3. Lazima salio lako la MPESA iongezeke kwa kiwango kilichotumwa mfano una 1,000 na ukatumiwa shs 500 lazima saliojipya la kwenye ujumbe uwe ni Shs 1,500/=

Kwa bahati mbaya nilipotaka kuripoti VodaCom kwa kupiga namba 100 nikakutana na matangazo mpaka nikakinai.

Kama kuna mtu anaweza shauri ni hatua gani za kuchukua kuripoti namba za kitapeli kama hizi atusaidie sote

Toa maoni yako juu ya Namna ya Kutambua Utapeli wa MPESA kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply