Pambano la Ngumi la Manny Paqcuiao na Mayweather 3 May 2015

0
923
Pambano la Ngumi la Manny Paqcuiao na Mayweather 3 MAy 2015
  • Floyd Mayweather amshinda Manny Pacquiao kwa points
  • Abakia bondia anayeshinda bila kupigwa 48-0
  • Kevin Mitchell: Mayweather ni mjanja mwenye bahati
  • Majaji wampa pointi 116-112, 116-112 na 118-110
  • Mayweather alirusha ngumi 435
  • Zilizotua kwa Manny Pacquiao 148 sawa (34%)
  • Manny Pacquiao alirusha ngumi 429
  • Zilizotua kwa Mayweather 81 sawa na (19%)
  • Floyd Mayweather atumia mbinu za kindondi kushinda

Floyd Mayweather amshinda Many Pacquiao katika pambano la karne kama ilivyotabiriwa. Hii inamfanya Mayweather kuendeleza rekodi yake nzuri ya kushinda mapambano yake ya 48-0

Paquiao alikuwa mkorofi mwanzoni wma pambano lakini kasi yake ilipungua sana katikati ya pambano na kuwafanya mashabiki wa Mayweather kutawala jukwaa kwa kushangilia.

Mayweather alitumia uzoefu mkubwa sana kujikinga na ngumi za Manny Pacquiao ambazo zilikuwa zikimiminwa sana lakini hata hivyo hazikufanikiwa kuingia kwenye ngome ya Mayweather

Majaji walitoa alama zifuatazo 118-110, 116-112, 116-112. Na kulingana na sheria za ngumi, maamuzi ya pamoja ya majaji ndio uamuzi wa mwisho.

Mayweather azuia ngumi 148 kati ya 435 alizorushiwa na Manny Pacqiao sawa ma (34%) wakati ambapo Manny Pacquiao alizuia tu 81 kati ya 429 sawa na (19%) alizorushiwa na May weather

Kadi ya kurekodia matokeo ya pambano kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacqiao 3 May 2015
Kadi ya kurekodia matokeo ya pambano kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacqiao 3 May 2015

Hata hivyo Manny Pacquiao hakuridhika na matokeo

“I thought I won the fight,” Pacquiao said after the fight. “He didn’t do nothing.”

“Nlidhani nimeshinda pambano” Pacqiao alisema mwishoni mwa pambano hilo. “Hakufanya kitu chochote”

Kambi ya Many Pacqiao wanadai kuwa bondia wao alikuwa ameumia began a ndio maana hakurusha ngumi nzito kama kawaida yake.

Akijibu shutuma hizo naye Mayweather alijibu kuwa naye alikuwa anaumwa, akakanusha kuwa hiyo sio kisingizio halali

Pambano hilo lilifanyika katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena, Las Vegas, Nevada tarehe 2 Mei, 2015 usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki

Bofya hapa Maelezo zaidi ya pambano la Floyd Mayweather na Manny Pacqiao 2 Mei 2015

Toa maoni yako juu ya Pambano la Ngumi la Manny Paqcuiao na Mayweather 3 May 2015 kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply