Prof Kitila Mkumbo Akataa Kugombea Kupitia ACT Wazalendo

0
458
Prof Kitila Mkumbo ACT Maendeleo

Katika barua yake aliyoiandikia kamati kuu ya ACT Wazalendo, Prof Kitila Mkumbo amesema kuwa hakubali uteuzi huo kwani hayuko tayari kisaikolojia, kifamilia na kisiasa kuchukua jukumu hilo.

Ikumbukwe kuwa Prof Kitila Mkumbo ni mojawapo wa wasomi wa kwanza kabisa kuusifia uamuzi mgumu wa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania Ndg Edward Lowassa kuhamia CHADEMA. Na pia huku ACT na CHADEMA hawapikiki chungu kimoja, Profesa Kitiula alikisifia CHADEMA kwa kumnasa mwanasiasa huyo mahiri mwenye mvuto ndani na nje ya CCM. Alidai kuwa Lowassa kuhamia upinzani kutabalisha kabisa historia na mwitikio wa kisiasa Tanzania tofauti na ilivyokuwa tangu 1992 wakati vyama vyingi viliporuhusiwa rasmi.

================================

Barua yenyewe ndio hii hapa:

Ndugu Wazalendo,
Naomba niwashukuru nyote kwa imani kubwa mliyo nayo juu yangu katika kukiwakilisha chama katika nafasi ya Rais. Naishukuru pia Kamati Kuu kwa imani yake kwangu hata kufikia hatua ya kupitisha azimio la kuniomba nigombee urais kwa chama chetu. Jana Kamati Kuu ilituma ujumbe maalumu nyumbani kwangu kwa ajili ya kuzungumza na familia na jamaa zangu juu ya ombi hili.
Aidha, Nimekuwa nikilitafakari jambo hili tangu Alhamisi nilipoombwa rasmi kutafakari uwezekano wa mimi kugombea baada ya juhudi zetu za kutafuta mgombea kushindikana. Nimefanya mawasiliano mapana katika familia, ndani ya chama, chuoni ninapofanyia kazi, Kanisani kwangu,na kwa watu na taasisi mbalimbali ninazohusiana nazo.
Baada ya tafakari na mawasiliano (consultations) mapana nasikitika kusema kwamba sina utayari na maandalizi ya maana ya kisaikolojia, kifamilia, na kisiasa kuniwezesha kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi huu.
Najua nimewaangusha sana katika uamuzi wangu huu lakini naamini kwamba mtaheshimu uamuzi wangu na kwamba hamtaacha kuthamini mchango wangu katika chama kwa sababu ya kukataa kugombea urais.
Nasikitika kwa tuhuma ambazo baadhi ya wanachama wetu wanarusha katika mitandao ya kijamii na sehemu zingine. Nathamini na kuheshimu haki ya wanachama wetu kuonyesha hasira kwa jambo wasilolipenda. Hata hivyo nawasihi wanachama wetu wajizuie kuzusha mambo yatakayochochea chuki ndani ya chama na kukatishana tamaa.
Nashauri tuwaombe wanachama wetu wengine waandamizi wachukue jukumu hili, wakiwemo mama mwenyekiti na Katibu Mkuu, kuwataja tu kwa uchache.
Tunapotafari haya, tusisahau Malengo Mapana ya chama chetu tuliyojiwekea katika uchaguzi huu. Ni bahati nzuri kwamba tumefanikiwa kuweka wagombea wa ubunge na Udiwani katika kata na katika majimbo mengi. Tusiyumbe.
Ahsanteni.
Kitila Mkumbo
17 Agosti 2015

Toa maoni yako juu ya Prof Kitila Mkumbo Akataa Kugombea Kupitia ACT Wazalendo kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply