Ripoti ya Mwakyembe Ililenga Uwaziri Mkuu wa Lowassa na Sio Ufisadi

0
695
Edward Loawassa ndani ya ITV

Ukitaka kujua kuwa Lowassa alikuwa mkweli kwamba Ripoti ya Mwakyembe ililenga kumchafua Lowassa ili aachie uwaziri mkuu ebu linganisha yafuatayo.

Tume iliyoongozwa na Dr Mwakyembe hakumhoji Lowassa kwa habari ya Richmond kwa sababu ilijua hakuusika na scandal na hii inadhibitisha kuwa hii scandal haikuwepo ila ilipikwa kwa ajili ya kumuondoa Lowassa kwenye uwaziri mkuu.

Ripoti ya Mwakyembe ilidai Richmond ni kampuni ya mfukoni na haikusajiliwa popote Marekani, mbona serikali ilipodai taarifa za usajili wa Richmond kutoka kwenye Ubalozi wa Marekani nchini walipewa taarifa kuwa Richmond imesajiliwa huko Huston, Texas kwa jina la Richmond Limited Liability Company (LLC)?

Ripoti pia ilidai kuwa mitambo iliyonunuliwa na Richmond ni feki na isingeweza kuzalisha umeme unaotakiwa. Sasa mimi anauliza kama ile mitambo ilikuwa ni mibovu kwa nini Wamarekani wanaopenda vitu quality wamenunua sisi Watz tukaachwa macho wazi tunaduwaa. Tena baada ya kununua watz waka shut up? kuna jambo hapo. Mitambo ambayo ilionekana mibovu na feki na hailingani na gharama ya milioni 60 ambayo TANESCO ilikuwa inunue kwa bei hiyo ilikuja kuuzwa kwa kampuni ya Kimarekani ya Symbion Power mbele ya Hilary Clinton na OBAMA na sasa inazalisha umeme kwenda mbele.

Wakati kashfa ya richmond inakuja onboard, IPTL wao walishabobea kwenye kupiga bingo ya capacity charge ya bilioni 5 kwa mwezi na mkataba wa zaidi ya miaka 20 huku mkataba ukilazimisha kulipwa capacity charge hata kama hawazalishi umeme. Kama akina mwakyembe hawakuwa wanaumezea mate uwaziri mkuu wa Lowassa kwa nini hawakuona hiyo ya IPTL? ambayo baadaye ndio ilikuja zaa ESCROW?

Kama akina Mwakyembe hawakuwa wanamezea mate uawaziri mkuu wa Lowassa kwa nini hawakuona kuwa Richmond ilisajiliwa Huston, Texas na kwamba mitambo iliyonunuliwa ilikuwa kwenye ubora wake mpaka wamarekani wakaipenda na kuinunua?

PAP iliyonunua IPTL bila hata kuwekeza chochote ambayo nayo usajili wake ni tata na kuhusishwa na kashfa ya Tegeta ESCROW Waziri mkuu wake (Pinda) ameachwa tu hivyo hivyo bora ya Lowassa aliyejiuzulu kwa kuwajibika

Ndio maana sasa namuamini Lowassa anaposema kuwa tatizo haikuwa richmond bali ni uwaziri mkuu

Hata sasa baada ya miaka 8 Lowassa akiwa nje ya serakali anasakamwa kwa staili ile ile ya mwaka 2008. Tatizo mimi nasema sio Richmond, kwa sababu ingekuwa ni ufisadi wa Richmond na ushahidi upo angepelekwa mahakamani kama akina mramba na wenzake. Tatizo hapa ni Urais. huu urais wa Tanzania wa kupeana kama kiti cha ufalme ndani ya ukoo wa kifalme (CCM)

Toa maoni yako juu ya Ripoti ya Mwakyembe Ililenga Uwaziri Mkuu wa Lowassa na Sio Ufisadi kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply