Sakata la Pinda ,Pengo na Gwajima Lafika Pabaya

0
1236

Kadinali Polycarp PengoWAJIMA AAMUA KUMTUSI KARDINALI PENGO MATUSI MAZITO.

kumbe kardinali PENGO alielekezwa na Mizengo PINDA Kutoa Tamko lake.

Wadau

Kuna mambo yanatimka na kuendelea huku Maofisini kwetu, yanakera, yanachefua na si ya kizalendo hata kidogo, na kila mpenda haki na amani lazima ayapinge kwa nguvu zake zote. Nimeona niyachomoe yaende hewani hivi hivi.

Jana Kumekuwa na Vikao vya ‘wakubwa selikalini ’ Kujadili tamko la Gwajima kwa Pengo, waziwazi wakubwa hao wametueleza kwamba wameelekezwa na Mizengo Pinda wamfuatilie Gwajima, kuanzia Usajili wa kanisa lake na sijui wamepanga nini zaidi. Maafisa Polisi wameagizwa kuanza ‘kazi’ ambayo hatujaijua bado kuhusu Gwajima, na maelekezi Yote yametoka kwa waziri Mkuu, Mh Peter Kayanza Pinda

Chanzo cha karibu kabisa na nyumbani kwa Pinda kinasema Pinda na Kardinali Pengo ni marafiki, na wamesoma Seminary pamoja, na wote ni wafipa. Chanzo kimesema bila kuogopa kwamba kumekuwa na kutembeleana kwa Pinda na Pengo kwa Mazungumzo, na chanzo kimetema wazi kwamba ni Pinda ndie aliye muelekeza Kardinali Pengo kwenda kinyume na matamko ya maaskofu Wote kwenye waraka ambao hata yeye Pengo aliusaini na kuukubali.

Chanzo kinasema pia kwamba Ni Pinda aliye mshawishi Pengo awaasi maaskofu wenzake na watu wa makanisa Yote. Chanzo kinadai binafsi kilikasirishwa sana na Kitendo cha Waziri mkuu kumnajisi kardinali pengo ambaye alikuwa na sifa kubwa ndani na nje ya nchi yetu.

Taarifa hizi ambazo zimesambaa kwa maaskofu wote wa Kanisa Katoliki wamemlaani sana Pinda, kitendo cha Pinda kumuharibu Pengo, na Kumfanya Pengo kama mtoto wa kuasi maamuzi yake mwenyewe kimewakera sana.

Baraza la maaskofu wa Katoliki linangoja kumuuliza Pengo, Ni kitu gani huyu Mfipa mwenzake alimlewesha kiasi cha kuropoka maneno hatari. Tamko la Gwajima kumrarua Pengo lilikuwa kumrarua Pinda ambae amekuwa mtoa maelekezo yale, sasa Pinda amekuwa Mbogo, ameanza kama chizi Kumsakama Gwajima, na Kutuharibia utaratibu wa kazi zetu za kila siku serikalini.

Baadhi ya maofisa wetu kwenye kikao walimjibu Pinda kwamba Askofu Pengo kashambuliwa na Askofu Gwajima waachwe maaskofu wapambane wao kwa wao bila kuweka mkono wa serikali kwenye mambo ya dini. Matamshi hayo yalionekana kumkera sana Pinda aliyemtishia nafasi yake.

Kuna chanzo kingine cha karibu sana ambacho kilirekodi kikao cha Pinda na Pengo. Kadiri ya sakata linavyoendelea kaeni mkao wa kuona Mengi. Kanisa la Gwajima jiandaeni kupokea ‘mambo’ kutoka kwa Pinda.
Natuma kama nilivyopata…

Toa maoni yako juu ya Sakata la Pinda ,Pengo na Gwajima Lafika Pabaya kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply