Ujio wa LOWASSA Upinzani na Maswali Mengi ya Ufisadi

0
1064
Na Kilasi Shama Michael

LOWASA CHADEMA

Maswali kwa UJIO wa lowasa chadema## Yapaswa kujiandaa kisaikolojia na tujifunze SIASA za kileo..politics is about people and their interest. .jiulize haya maswali 10?

1. Nyerere alitabiri kuwa CHADEMA ndio chama kitakachopokea kijiti cha CCM Aliona mbali, JE hii unakubali?

2. Nyerere alitabiri na alisisitiza upinzani wa kweli utatoka CCM, Mfano lulu ya CHADEMA dr slaa alitoka CCM, Je unafahamu kuwa Lowasa ametoka CCM na ana nguvu mara 10 ya Dr slaa?

3. Lowasa aliwahi kusema mwenye ushahidi na tuhuma yeyote ya ufisadi ampeleke mahakamani kama CHADEMA tunaamini alikuwa fisadi je milango ya mahakama hatukuiona?

4. Lowasa na kashfa ya kuiuza CHADEMA, Je unafahamu kuwa atagombea URAIS na sio uenyekiti wa chama na atasmamiwa na chama kama atafuata misingi na taratibu za chama?

5. Wagombea wakuu watakua ni MAGUFURI NA LOWASA, Je kama wewe ni mpenda mabadiliko na haumtaki lowasa unaona ni bora ukamchague statistician Magufuri na sio Kamanda mpya?

6. Wengi wetu tumeipenda CHADEMA kwa misimamo ya viongozi wetu wasioteteleka na tumewaamini kwa miaka Mingi, Je unadhani wao hawajaangalia faida na hasara za kumpokea LOWASA? Kwanini wampokee?

7. Tujitoe ufahamu kuwa CHADEMA wamekosea kumpokea Lowasa, je unadhani CUF, NCCR na NLD nao wamekosea au wamelogwa?

8. Unafahamu kwamba Vyama vingi vilivyoleta uhuru Africa vilipinduliwa na wanaharakati waliotoka huko? Kwann tusikubali fahari tuliyopewa na Mungu

9. Unakumbuka Kikwete alizikataa kura za walimu 2010 na ndio zilitubeba Dr Slaa alipoziomba, leo Lowasa ndio mwanasiasa mwenye nguvu kuliko WanaCCM wote ndani ya CCM na ndio mwenye nguvu kuliko wapinzani wote nje ya CCM, je kura zinazotokana na huyu tufanye kosa la kuzikataa kama kikwete?

10. Mfumo wa CCM ni wa kifisadi hata msafi atapakwa matope na mchafu atasafishwa, Mfano tungemkataa Dr slaa alipotoka CCM kwa tuhuma alizozipata akiwa padre Je leo na 2010 nani angegombea urais?

Ifike kipindi tusiwakosee heshima viongozi wetu, kwa hili moja tukaona tunajua kuliko tuliowaamini. Adui wa Taifa Hili sio mtu au watu ila ni CCM..tuhuma sio ushahidi hata CHADEMA tulipata hati shaka kutoka kwa CAG..Magufuri ndio mwenyekiti wa kwanza wa chama atakae kuwa sio Rais wa tz.

JE WIZI NI MFUMO WA CCM AU NI LOWASA.?

Uikileta tunda na kulidondosha kwenye uchafu utaliita uchafu lakini mtu akiliikota akalisafisha vizuri kinakuwa chakula.

Leo hii mtu yeyote akiwa ni mzuri lakini anatumika ndani ya mfumo wa CCM uliojaa mambo ya kifisadi
na wizi wa rasilimali za taifa utamuita mwizi hata kama hajaiba yeye kwa sababu CCM wana tabia ya kuficha maovu na kuficha majina ya watenda maovu au kuwalinda.

Mfumo wa ccm una mambo mengi mabaya yaliyojificha kwenye migongo ya watu wema.

Mfano ni nani wa kuthibitisha kwamba,Balali alikufa?

USHAIDI

– Je, wakati fedha za Mkonge kupitia mfanyabiashara aitwaye CHAVDA zinaibiwa Lowassa alikuwa waziri mkuu? Alikuwa malecela!.

– Madini ya dhahabu yaliyokamatwa uwanja wa ndege wakati wa Rais Mwinyi yalikuwa ni madini ya Lowassa?

– Wakati Akasha wa dawa za kulevya anakamatwa na kutoroshwa aliyehusika ni Lowassa? Waziri Mkuu alikuwa Malecela.

– Mrema alipolipua bomu la mwenyekiti wa CCM kuhongwa milioni 900 za minofu ya samaki alikuwa ni Lowassa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye .

– Kashfa ya sukari alikuwa ni Lowasa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye.

– Kashfa ya Loliondo gate 1992 ya mtoto wa mfalme wa Kuwait alikuwa ni Lowassa? Kinana na Abubakar Mgumia walihusika.

– Wanyama hai kutoroshwa nje ya nchi alikuwa Lowassa? Waziri mkuu Pinda.

– EPA aliyeidhinisha fedha zichukuliwe alikuwa Lowassa? Mkapa na Mangula wanajua.

– NBC Bank kuuzwa alikuwa Lowasa? Mkapa na Sumaye wanahusika.

– Kiwira alikuwa Lowassa? Mkapa na Sumaye wanahusika.

– Rada na ndege ya rais alikuwa Lowassa? Mkapa, Chenge na Dr. Rashid walihusika.

– Mkataba wa Buzwagi alikuwa Lowassa? Karamagi,Kikwete na Mwakapugi walihusika.

– Stimulus package ya wakulima wa pamba baada ya Mdororo wa uchumi duniani alikuwa Lowassa? Kigwangala na Kikwete wanajua.

– Fedha za Bunge la Katiba zilizobaki baada ya UKAWA kususia Bunge hilo bilioni 3.87 alizichukuwa Lowasa? Sitta, Samia suluhu wanahusika.

-Bilioni 250 zilizolipwa wakandarasi hewa wa ujenzi wa barabara alikuwa Lowassa? Magufuri na Tizeba wanahusika.

– TTCL Kuuzwa kwa bei ya kutupa kwa Celtel alikuwa ni Lowassa? Mwandosya analo jibu.

– Mabehewa mitumba zilizonunuliwa alikuwa ni Lowassa? Mwakyembe anahusika.

– Kashfa za pembejeo za wakulima alikuwa ni Lowassa? Wassira na Pinda wanahusika.

– Fedha za Gadaffi alikuwa ni Lowassa? Alikuwa ni Membe.

– Ununuzi wa nyumba ya Ubalozi wa Tanzania Italia alikuwa ni Lowassa? Kikwete na Mahalu wanahusika.

– Escrow tegeta account alikuwa ni Lowassa? Kikwete, Muhongo, Maswi, Albert Marwa wanahusika

– Mradi wa malaria no more alikuwa ni Lowassa? January Makamba mhusika.

Toa maoni yako juu ya Ujio wa LOWASSA Upinzani na Maswali Mengi ya Ufisadi kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply