Vichekesho Mkutano wa Mandela na Nyerere Kule Ng’ambo ya Pili

1
16630
Vichekesho vya Nyerere na Mandela

:  Kama vile nakufananisha?
Mandela: Hata mimi naona sio sura ngeni?
: We ndie Mandela eee?!
Mandela: Ndiyo mimi haswa miaka 14 ni mingi.
: Sana!!.
Mandela: Sasa nitakaa wapi mbona hakueleweki huku?
Nyerere: We ngoja utapaelewa tu.
Nyerere: Eeh!! vipi huko ? ulitembelea hata hivi karibuni?

Mandela:

Eeeh! we acha tu, huko mara Zitto msaliti, mara Umeme mgawo miezi sita, mara mgomo wa Gesi haitoki Mtwara, mara kifo cha Mwangosi, mara Dawa za Kulevya,  mara Meno ya Tembo, mara kuchoma Makanisa, mara mabomu kwenye mikutano ya hadhara na makanisani, mara  , mara Dr. Ulimboka na Kibanda kung’olewa kucha na meno kwa plauzi, mara Division 5, mara Udini, mara ngumi Bungeni, mara kifo cha Dr Mvungi, mara tindikali kwa mapadri, mashehe na wageni, mara Kagame kuishambulia Tanznia, Petroli kuchakachuliwa, mara wengine wanasema eti Muungano ulioasisi unatokana na Visiwa vya Zimbabwe na Zanzibar na sio Tanganyika tena, mara muungano wa serikali tatu ndio unaotakiwa, mara Kigamboni kapewa Obama, mara Bushi na mke wake kaja , Clinton na mke wake kaja , Kamerun na mke wake kaja , Xiing wa uchina kaja , mara puttin wa Urusi kaja . Yaani hekaya ni ndefu bora urudi ukayashuhudie mwenyewe.

Mara Mandela alipomrushia macho swahiba wake kumbe kashazimia saa nyingi

Toa maoni yako juu ya Vichekesho Mkutano wa Mandela na Nyerere Kule Ng’ambo ya Pili kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Oni moja

ACHA MAONI

Please enter your comment!
Please enter your name here