Vichekesho vya Mume na Mke – Penzi la Pesa

2
5913

MUME: Hallo my queen…

MKE: Nambiee..my darling

MUME: Nimekumiss honey.

MKE: Hata mie nimekumiss ile mbaya..

MUME: Samahani mke wangu leo sitaweza kurudi nyumbani.. nitakuja kesho asubuhi

MKE: Unasemaje?? na uishie hukohuko.. kalale kwa hao mahawara zako.. mwanaume mbaya wewe, kama sokwe.. sijui hata ni shetani gani alienishawishi hadi nikaolewa na sokwe kama wewe..

yaani najuta.. najuta.. sikupendi toka ndani ya moyo wangu..

sikupendi hata kidogo..naogopa hata watu kujua kuwa umenioa ..

naona aibu.

MUME: Punguza jazba mke wangu niko bank.. kuna foleni ndefu sana..

MKE: Ahh pole sana darling.. nakuonea huruma handsome wangu wa kipekee.. but baby usisahau kuniletea pesa kidogo.. ninashida na laki 2, alafu kuna ile elfu 70 anayonidai
mama amina leo alikuja kunikumbushia. nimekuandalia maji ya moto sweetie ukija uoge mume wangu kipenzi.. then ukumbuke kuniletea chips na kuku wa kuchoma gengeni.. nimeimiss sana.. nakupenda sana mfalme wangu..

MUME: Ni bank ya kuchangia damu.

MKE: Na wakutoe hiyo damu yote, bora ufe tu.. huna faida na si lolote.. nyooo… potelea mbali..mijitu mingine bhana..!!

Toa maoni yako juu ya Vichekesho vya Mume na Mke – Penzi la Pesa kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

2 COMMENTS

Leave a Reply