Vifo vya Wafanyakazi Wakidai Haki Yao

1
1671
Wafanyakazi wa Migodi ya Madini Wakiandamana Afrika ya Kusini

Wafanyakazi wa Migodi ya Madini Wakiandamana Afrika ya KusiniWafanyakazi wa migodi ya dhahabu ya Lonmin’s Marikana platinum mine, Rustenburg, km kama 100 kaskazini magharibi mwa Johannesburg waliingia kwenye mgomo na maandamano ya kudai nyongeza ya mishahara mnamo tarehe 16 Agosti 2012. Katika kukabiliana na mgomo huo polisi waliwafyatulia risasi za moto waandamanaji na kuwaua takriban 34 na kuwaacha wengi wakijeruhiwa.

Mauaji haya yanawakumbusha raia wa Afrika Kusini mauaji ya ubaguzi wa rangi yaliyokuwa yakitekelezwa kwa amri ya chama cha makaburu wakati huo, ila tofauti na haya ni kuwa mauaji yametekelezwa chini ya chama cha ANC ambacho ndicho kilichowaongoza Waafrika hao kudai uhuru halisi. Tena mauaji yametokea ndani ya utawala wa Jacob Zuma kiongozi aliyeingia madarakani kwa nguvu ya walalahoi wa Afrika ya Kusini.

Akijibu tuhuma za mauaji hayo, mkuu wa polisi Riah Phiyega alidai

Tulifanya tulichoweza kufanya. maaskari wetu wa Marikana, walinzi wawili, msimamizi mmoja na maofisa wawili walitekwa na walikuwa katika hatari ya kuuliwa na waandamanaji waliokuwa wamebeba mishale, marungu na mapanga

Hayo yametokea baada ya mgomo wa takriban wiki nzima na mikusanyiko iliyokuwa ikifanywa na hao wafanyakazi katika “Kilima cha Kutisha” kama ilivyobatizwa jina na vyombo vya habari nchini humo.

Msemaji huyo wa polisi aliendelea kudai kuwa wanao ushahidi kuwa baadhi ya wanamgomo hao wametumia uchawi maarufu unaitwa “MUTI” ili kupata ujasiri wakati wa vita. Kwamba uchawi huo ungewapa kinga dhidi ya polisi na risasi yeyote isingewadhuru.

Akiongea na shiraka la utangazaji la REUTER, taarifa hiyo ilisema kuwa helikopta ya polisi imechukua picha ikimuenyesha huyo “sangoma” mganga wao akiwapa upako huo baadhi ya hao wafanyakazi.

Taarifa za polisi kwa ujumla zinaonyesha kuwa hao waandamanaji ni hatari na wangeweza kufanya chochote kwa polisi ikiwa ni pamoja na kuwaua polisi.

Kwa upande wao mmoja wa waandamanaji Lazarus Letsoele, alidai kuwa polisi walianza kuwatawanya wafanyakazi hao kwa kutumia wavu mkubwa kuelekea upande wa chini wa mlima. Pia alidai kuwa ni kweli wafanyakazi walikuwa na silaha za kujilinda kama bastola na marungu.

Baadhi yetu tulikuwa na silaha, lakini kwa ajili ya ulinzi binafsi na sio kuwashambulia polisi”, Letsoele  alisema

Kwa maelezo zaidi tembelea hapa

National Posts

Toa maoni yako juu ya Vifo vya Wafanyakazi Wakidai Haki Yao kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Oni moja

Leave a Reply