Kuna Shida Gani Watoto wa Vigogo Kuwaridhi Wazazi Wao?

0
2001
Kuna Shida Gani Watoto wa Vigogo Kuwaridhi Wazazi Wao?
Kuna malumbano yamewahi na yanaweza kuendelea kutokea kwamba je ni haki au sio haki watoto wa vigogo kufuata nyayo za baba zao au mama zao hasa kwenye siasa.
Wakati Nyerere aliiweka mbali familia yake isijinufaishe na siasa kwa sababu ya yeye kuwa kwenye siasa na uongozi, takriban viongozi wote wa zamani na sasa ndani ya CCM ya leo wanatumia fursa walizonazo kuhakikisha baadhi kama sio wote wa watoto wao wanapata nafasi nyeti ndani ya chama na serikali. Pia kuna wengi japo wazazi wao hawakuhusika na kuwapachika watoto wao kweny nafasi nyeti za kisiasa lakini vimvuli vya vyenye nguvu imeweza kuwafanya viongozi wa sasa wa CCM kuwakumbuka na kuwaweka haraka haraka kama familia za akina Nyerere, Sokoine, Nnauye, Kawawa nk.
 Wapo wengi tunaweza kuwataja wengi wao wamekwisha fariki na wachache bado wako hai
Najua nyakati zile za ujamaa na kujitegemea zimeshapita na pengine kupitwa na wakati. Sasa tupo nyakati za Ubepari na Kujitegemea tukiongozwa na utanda wizi  wa digitali
Hebu tuseme ukweli
Je ni vibaya kwa watoto wa vigogo kufuata nyayo za baba zao na mama zao katika siasa na uongozi wa umma? Je hapo hakuna mgongano wa kimaslahi? Kama ni sawa basi ina maana Nyerere alikuwa na makosa? Na wazazi wetu waliofuata kwa uaminifu wa siasa za Ujamaa na kujitegemea waliingizwa mjini? wakafa mafukara wa kutupwa
Twende taratibu; kama Nyerere alikuwa sawa, sasa hawa CCM na wengineo waliowaridhisha watoto wao viatu vyao vya siasa uongozi wa umma tuwaweke wapi?
Mimi binafsi sioni ubaya endapo mtoto ataamua kuingia kwenye siasa na kuamua kuwapinga wazazi wao kama akina Makongoro Neyrere walivyofanya baada ya kuibukia upinzani katika  miaka ya tisini.

Mfano wa watoto wa vigogo kuibukia siasa za wazazi wao ni

Nape kafuata nyayo za babake marehemu, mzee Moses Nnauye

Angela Kairuki kufuata nyayo za mama Mkwizu
January Makamba  kufuata nyayo za babake Makamba Mzee wa Kurhani na Biblia (Katibu mkuu mstaafu wa CCM)
Dr Mathayo David Matahayo kufuata nyayo za Cleopa David Msuya (Waziri mkuu mstaafu)
Hussein Mwinyi kufuata nyayo za Alhaji Hassan Mwinyi (Rais Mstaafu wa pili wa Tanzania)

Wengine ni:

Gerald J. Guninita
Paul Mzindakaya

Festo Kiswaga
Khanifa M. Karamagi
Husna Mwilima

John V. K. Mongella
John B. Henjewele
Agnes Hokororo
Vita Kawawa
Zainabu Kawawa
Adam Kighoma Malima
E Sokoine
Nape Nnauye
Dickson Membe
Fredy Lowasa
Ridhiwani Kikwete
Ashura Hussein Mwinyi
Ben Samwel Sitta
Debora Mwandosya
Irene Pinda
Felister Ndugai
Christopher Ndejembi
Sharifa Bilal
Hawa Kigoda
Judith Mukama
Jalome Msekwa
Mboni Mhita
Jonas Nkya

Kutoka Mitandao Mingine

Bumbuli Development Corporation (BDC) | Facebook
https://www.facebook.com/BumbuliDevelopmentCorporation
Bumbuli Development Corporation (BDC), Dar es Salaam, Tanzania. Fikiria watoto wa vigogo kujaa kwenye ofisi nyeti za umma huku hata abc za kazi 

UVCCM imegeuka ‘klabu maalumu’ ya watoto wa vigogo?
http://www.raiamwema.co.tz/uvccm-imegeuka-%25E2%2580%2598klabu-maalumu%25E2%2580%2599-ya-watoto-wa-vigogo
17 Okt 2012 Tukirejea kwenye umoja huo wa vijana wa CCM, itashangaza kuuona umoja ambao ngazi yake ya juu imejaa watoto wa vigogo na wa matajiri, 

Msema Kweli
http://pwanihalisi.blogspot.com/
Nov 23, 2012 TUMESHUHUDIA Mkutano Mkuu wa nane wa CCM ukimalizika kwa vigogo wanaotarajiwa kukivusha kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. …. 8 ya watu wazima walisema kuwa watoto wao walipewa chakula wakiwa 

 

Toa maoni yako juu ya Kuna Shida Gani Watoto wa Vigogo Kuwaridhi Wazazi Wao? kwa kutumia nafasi hapo chini ilipoandikwa ACHA MAONI

Leave a Reply